Timu zote mbili zikisalimiana
Salaam
Picha ya pamoja ya Waaamuzi wa Kagera Sugar na Mbeya City
Timu Kapteni na waamuzi wakiteta kabla ya mtanange
Picha ya pamoja

Kikosi cha timu ya Kagera Sugar kilichoanza
Kikosi kilichoanza cha Mbeya City

Kikosi cha Mbeya City kikiomba leo katikati ya uwanja muda mfupi kabla ya mtanange kuanza

Hapa kazi tu!!! Twende tuanze mtanange kwa pamoja!!
Taswira kabla ya mtanange kuanza

Mashabiki wa Soka wamejitokeza kwa wingi leo

Taswira ya watazamaji Kaitaba leo hii

Mashabiki wa Mbeya City wakiutazama mpira leo Kaitaba mapema kipindi cha kwanza

Hapa ni ushindi tuu ...tunataka .....hatukuja kutafuta sare!!! ilisikika nyimbo kutoka kwa mashabiki!!!
Wakina dada nao walikuwemo...ngoma kutoka Mbeya
mpaka Kagera!!

Karibu Mbeya City Bukoba

Patashika zikiendelea uwanjani

Kutokana na Marekebisho ya Uwanja wa Kaitaba, wadau wakiwa safi kwenye siti zao kuangalia mtanange wa Kagera Sugar na Mbeya City

Mchezaji wa Mbeya City Deus Kaseke akiendesha hapa baada ya kuwatoka mabeki wa Kagera Sugar

Ilikuwa ni kazi kuingia kwenye eneo la box katika
mtanange huu

Kipa wa Kagera Hannington ameumia mguu na amelazimika kutoka nje ya uwaja na nafasi yake kuchukuliwa na kipa Adam Oseja

Hannington akitoka nje ya Uwanja baada ya kuumia

Ilimchukua muda na baadae watoa Huduma walimtoa baada ya kuona hajiwezi katika kutembea na kwenda
kumpa huduma ya kwanza nje ya uwanja.
Mbeya City wakifanya mabadiliko
Patashika kuutafuta mpira

Chupu chupu kipa
wa Mbeya City afungwe hapa katika kipindi cha pili

Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia bao lao lililofungwa na Richard Peter katika dakika ya 72 kipindi cha pili.

Richard
Peter akipongezwa na mwenzake baada ya kufunga bao na kuiwezesha Mbeya
City kuwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.

Wachezaji wa
Mbeya City wakirudi uwanjani baada ya kupata bao

Ubao Wenyeji kagera Sugar 0-1 Mbeya City

Mashabiki wa Mbeya City nje ...usiseme angalia walivyokuwa wanatupia....kanyaga ...chinja!!

Hapa kipa wa Mbeya City nae aliumia lakini aliweza kuamka
na kuendelea na kabumbu kama kawa!!

Mashabiki wa Mbeya City wakiuzunika baada ya kipa wao kuumia!

Mashabiki wa kagera
Sugar hoi baada ya kujionea kichapo hicho cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City.

Huku Majanga!!! huko vipi!!!

Kocha
wa Mbeya City Juma Mwambosi akiongea na mwandishi wa TBC1 kwenye uwanja
wa Kaitaba baada ya mpira kumalizika Kagera Sugar wakiwa hoi kwa
kichapo cha bao 1-0.

Kocha wa Mbeya City Juma Mwambosi

Baada ya mtanange kumalizika wachezaji wote wa Mbeya City wakifanya mazoezi kama vile mtanange ndio unaanza !!

Chinja ....chinja za Mbeya City!!!

Hakunaga!!! Kama Mbeya City...angalia Furaha zao hapa kwa kuinyoa Kagera Sukari leo

Furaha za ushindi zikiendelea Kaitaba ...

Kocha Juma Mwambosi nae hapa aliipongeza timu yake
Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU
ya Mbeya City leo imeanza msimu wa pili vyema baada ya kuifungia Kagera
Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani kaitaba bao 1-0. Kipindi cha kwanza
kilimalizika kikiwa hakuna timu iliyokuwa imeziona nyavu za mwenzake
hivyo zikalazimika kwenda mapumziko zikiwa 0-0, Huku kipa wa Kagera
Sugar Hannington akiwa hoi kwa kuumia mguu baada ya kuachia frii kiki na
kushtuka mguu na kulazimika kutolewa nje katika kipindi hicho cha
kwanza. Kipindi cha pili dakika ya 72 Mbeya City wamepata bao kupitia
mchezaji wao Richard Peter aliyekuwa amevaa jezi no. 13 mgongoni.
No comments:
Post a Comment