Search This Blog

Saturday, January 4, 2014

THE 11 –PROGRAMU YA KUZUIA AU KUEPUSHA MAJERAHA MICHEZONI/SOKA Pengine Umewahi kusikia mtu ambaye amewahi kuumia . Mchezo wa soka ni mchezo ambao una hatari ya kumletea majeraha mtu anayecheza. Lakini habari njema ni kwamba utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa matukio ya kuumia katika soka kunaweza kupunguzwa kwa progammu maalum za kuzuia majeraha kwa wachezaji.
11 ni proggramu rahisi na yenye kutumia muda mfupi ya kumuepusha au kumkinga mchezaji na majeraha ambayo inajumuisha mazoezi kumi ambayo yana ushahidi unaoonyesha jinsi inavyofanya kazi. 

11 ni progranu inayolenga kuongeza uungwana yaani FAIR PLAY latika mchezo na haihitaji kitu kingine cha ziada zaidi ya mpira na inafanywa kwa muda usiopungua dakika 10 mpaka 15 . Programu hii ni ya uhakika kuliko mazoezi mengi ambayo wachezaji huyatumia na inaweza kutumika katika nafasi ya mazoezi mengine.

Mazoezi yaliyopo katika programu hii yamejikita kwenye mbinu maalum za ambazo makocha wanapaswa kujifunza na kuzizoea ili waweze kuwapa wachezaji ili waweze kujenga misuli hasa ya mapaja pamoja na kumudu mnyumbuliko wa misuli kuendana na kasi ya mchezo. 

Moja ya mazoezi haya ni jinsi ya kujenga misuli kunyooka na kuwa thabiti.
Kanuni na programu hii ya 11 inatakiwa kufanywa kila siku katika wakati wa mazoezi ya wachezaji hasa baada ya kupasha mwili moto na kunyoosha misuli . Ili kuhakilisha uhakika wa mazoezi haya yanatakiwa kufanywa kama inavyotakiwa bila kukosea na kabla ya mechi unapaswa kuyafanya mazoezi haya kwa ufupi ili misuli isikakamae.

Programu hii ilianzishwa na kuendelezwa na FIFA katika idara yake ya afya na utafiti kwa ushirikiano na kundi la wataalamu wa kimataifa wa masuala ya afya michezoni . Baada ya kufuata programmu hii mchezaji ataongeza kiwango chake cha kuperform na kupunguza uwezekano wa kupata majeraha .

No comments:

Post a Comment