Search This Blog

Thursday, January 23, 2014

TANZIA: FUNDI WA VIFAA VYA TENNIS GYNKHANA CLUB NDUGU CHARLES KIANDO AFARIKI DUNIA



Siku chache baada ya kumazilika kwa Mashindano ya vijana ya Tennis ukanda wa Afrika Mashariki Kati,kwenye viwanja vya GhymKhana Jijini Dar-es-salaam,Tasnia hiyo imepata pigo baada ya Fundi Mkuu wa vifaa vya Tennis Kutoka Klabu ya Gymkhana Charles Kiando kufariki Dunia.
Charles Kiando Maarufu kama Tola,amefariki Dunia Alfajiri ya Leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipopelekwa baada ya kuzidiwa Ghafla,na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Mwananyamala Kwa Ali Maua Jijini Dar-es-salaam.
Clouds TV ilifanya nae mazungumzo enzi za Uhai wake,ili kuufahamisha UMMA wa Tanzania juu ya umuhimu wa Fundi huyo Mkongwe mkongwe kwa takribani miaka ishirini sasa.
Clouds Media Group,inaungana na wadau wote wa Michezo Tanzania,kutoa pole kwa familia ya Marehemu kwenye kipindi hiki kigumu,Mungu Amlaze mahala Pema Peponi Amin.

No comments:

Post a Comment