Search This Blog

Wednesday, January 8, 2014

SHEDRACK NSAJIGWA AACHANA NA UKOCHA,AREJEA TENA DIMBANI KUCHEZA SOKA LA KULIPWA,YUPO NCHINI NEPAL PAMOJA NA MSHAMBULIAJI PIUS KISAMBALE

Nahodha wa zamni wa Yanga na Taifa Stars Shedrack Nsajigwa ameandika historia baada ya kuachana na ukocha na kurejea tena uwanjani kukipiga.
Nsajigwa pamoja na mshambuliaji Pius Kisambale wanaichezea timu ya SARASWOTI YOUTH CLUB inayoshiriki ligi kuu ya nchini Nepal,
Hivi karibuni wachezaji hao waliisaidia timu yao kupata pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya RCT CLUB  kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini NEPAL.
Pius Kisambale ndiye aliifungia timu yake bao la kuwasazisha baada ya kupiga mpira wa adhabu ulioenda moja kwa moja kimiani.No comments:

Post a Comment