Search This Blog

Wednesday, January 22, 2014

REAL MADRID YAINGIA KWENYE MBIO ZA KUMSAJILI ROONEY.

Taarifa kutoka jijini Madrid zinasema mshambuliaji Wayne Rooney ameingia kwenye orodha ya washambuliaji wanaowataka mwishoni mwa msimu.
Huku mkataba wa Rooney ukiwa umebaki miezi 18 na inavyoelekea hana nia ya kuongeza mkataba mpya  pia klabu ya Manchester Utd haipo tayari kumuuza Rooney kwa vilabu vya England.
Kwenye orodha ya majina ya washambuliaji wanaotakiwa na Real Madrid ukiacha jina la Rooney ni Radamel Falcao na Kun Aguero
Sababu inayompa nafasi kubwa Rooney kusajiliwa na Madrid ni uwezo wake kucheza nafasi mbali mbali ukiacha nafasi ya ushambuliaji pia kocha wa sasa wa Madrid Carlo Anceletti anamfahamu vizuri katika kipindi alichokuwa anaifundisha Chelsea.
Kama Rooney atafanikiwa kujiunga na Madridi msimu ujao basi atajiunga tena na mshambuliaji Cristiano Ronaldo waliyekuwa pamoja kwenye klabu ya Manchester Utd.

No comments:

Post a Comment