
Leo ni ile siku ambayo ilikua ikisubiriwa kwa hamu na wakazi wa 88.5 Dar es salaam siku ya kilele cha miaka 14 ya Clouds Fm ambapo timu ya Clouds Fm ilianza sherehe hizi kwa kutembelea watu wenye matatizo mbalimbali.
Miongoni
mwa sehemu zilizotembelewa leo ni pamoja na Hospital ya wilaya ya
Temeke kisha kuelekea kwa jamaa ambaye anamiliki kituo cha kulea watu
walioathirika na madawa ya kulevya kiitwacho Keko Machungwa Youth Centre
ambacho kipo Keko Machungwa na mmiliki wa kituo hicho ni Yohana au Ctn
kama wanavyomwita.
Baada
ya hayo kukamilika ndipo timu ikasogea viwanja vya Mwembe Yanga ambapo
umati mkubwa wa watu wa rika mbalimbali walijitokeza kufurahi pamoja na
familia ya Clouds FM ambayo ilikua pale.
Jukwaa lilimilikiwa na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva ikiwa ni pamoja na Rich Mavoko,Fid Q,Makomando,Barnaba,Linex,Chegge na Temba,Mkubwa na wanawe,Madee,Shettah na wengine kibao.
Hizi ni baadhi ya picha za kilicho-happen MwembeYanga kwenye sherehe za Miaka 14 ya Clouds Fm











Source: millardayo.com

No comments:
Post a Comment