Search This Blog

Monday, January 20, 2014

MALINZI AELEZEA MIKAKATI YAKE KWA LOWASSA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.

Malinzi ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Amesema uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu.

Kwa upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.

CAPTION: Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake katika kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo umefanyika leo (Januari 20 mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es Salaam.

2 comments:

  1. Halafu iweje?mbona tangu achaguliwe hajakwenda kumweleza rais wala waziri wa michezo hiyo mikakati?ameanza kuingiza siasa kwenye mpira na haya ni maandalizi ya kumpigia kampeni Lowasa kupitia TFF,kama alivyofanya makanisani,misikitini na bodaboda.Ndio maana alikuwa wa kwanza kumpongeza Malinzi.Baada ya hapo tutashuhudia akialikwa kuwa mgeni wa heshima kwenye mechi kubwa kubwa zikiwemo za timu ya taifa

    ReplyDelete
  2. Afu huyu mng'ang'ania urais na michezo wapi na wapi jamani! Kweli tutayaona mengi mpaka 2015 October ipite

    ReplyDelete