Search This Blog

Tuesday, January 21, 2014

KISHONGOLE, KESSY KUSIMAMIA MECHI ZA CAF


Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Watanzania Alfred Rwiza Kishongole na Lina Kessy kuwa makamishna wa mechi za shirikisho hilo zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 mwaka huu.

Kishongole ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Cote d’Or ya Shelisheli na Kabuscorp de Palanca ya Angola.

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mchujo itafanyika Shelisheli na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Abdoul Ohabee Kanoso. Waamuzi wengine ni Basile Alain Rambeloson, Augustin Gabriel Herinirina na Andofetra Avombitana Rakotojaona.

Naye Kessy atakuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Rwanda na Kenya itakayochezwa jijini Kigali.

Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Cameroon. Mwamuzi wa kati ni Sylvie Abou wakati wasaidizi wake ni Winnie li Koudangbe, Lum Rochelle na Jeanne Ekoumou.

No comments:

Post a Comment