Search This Blog

Monday, January 13, 2014

HANS VAN DER PLYUM KUINOA YANGA

Hans Van Der Plyum ameingia mkataba wa kuinoa Young Africans kuanzia leo na moja kwa moja kesho mchana ataungana na wachezaji wake waliopo nchini Uturuki kwenye kambi ya mafunzo ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa baadae.
Kocha huyo mwenye mafanikio makubwa nchini Ghana aliwasili nchini Tanzania juzi na leo kumalizana na uongozi wa klabu ya Young Africans kisha usiku huu kuanza safari ya kuelekea nchini Uturuki kuungana na timu yake mpya ambayo ipo katika kambi ya mafunzo kwenye jiji la Antlaya.
Uongozi wa Young Africans umefikia hatua hiyo baada ya kuridhika na wasifu na rekodi yake na kuwa kocha pekee aliyeweza kuushawishi uongozi na kumpa kazi kutoka katika maombi mengi ambayo yalikuwa yametumwa na yakiendelea kumiminika kuomba ajira katika klabu kongwe nchini Tanzania.



Kuajairiwa kwa mholanzi Hans Van Der Plyum kunafunga mjadala juu ya nani anakua mrithi wa Ernie Brandts ambaye alisitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka jana na kumalizana na uongozi wa klabu ya Yanga kabla ya kurejeja kwao nchini Uholanzi.
Akiongea na mtando rasmi wa klabu ya Young Africans SC mwenyekiti wa kamati ya mashindano Abdallah Bin Kleb amesema kwa pamoja wamekubaliana baada ya kurizika na uwezo na rekodi yake ambayo wanaamini itasaidia kuipeleka timu katika hatua nyingine.
Sisi tumeamua kuingia mkataba na kocha Van der Plyum ili aweze kuisaidia timu yetu kutoka katika hatua iliyo na kwenda mbele zaidi, mtazamo wetu mkubwa ni katika mashindano ya kimataifa hasa Klabu Bingwa kwa kushirikiana na kocha msaidizi mzoefu mwenye elimu ya juu pia ya ukocha nchini Mkwasa tunaamini tufanya vizuri katika Ligi Kuu na Klabu Bingwa Afrika.
Aidha Hans Van der Plyum amesema anashukru uongozi wa Young Africans kwa kumuamini na kumpa nafasi hyo na kuahidi kwa kushirikiana na kocha Mkwasa na Pondamali ambao atakutana nao Uturuki watakiimarisha kikosi na pindi kitaporejea nchini kitakua katika hali nzuri na kucheza soka safi.
Pia kocha huyo mholanzi amesema anamjua vizuri kocha mkuu wa Simba SC Zdravko Logarusic kwani mwaka 2011 alikua akifundisha timu ya Ashanti Gold SC nchini Ghana na walipokutana katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya timu yake ya Berekum Chelsea aliweza kuibuka mbabe kwa kuifunga timu ya Ashanti mabao 4-0.

 Huu ndo Wasifu wa Hans Van Der Plyum:
CAREER DETAILS
Playing Career
• 18 year goalkeeping career in Eredivisie (Dutch Premier League) and Dutch First Division 
• 1965-1967 Wilhelmina SC
• 1967 – 1985 Den Bosch FC
• 1971 Goalkeeper of Dutch National Under-23 Team
Trainer/Coach
• Dutch Eredivisie and First Division
Head Coach:
FC Den Bosch (1993 -1997), Excelsior Rotterdam (1997 – 1998) 
Youth/Reserve Team Coach and Assistant First Team Coach:
FC Den Bosch (1990 – 1993)

• Ghana Premier League
(Ashanti Goldfields SC [Now AshantiGold](1998-2001, 2004 -2005), Heart of Lions FC (2002-2003, 2006 – 2007 2010 –2011) , Kessben FC (2008 – 2009) Berekum  Chelsea  (2011 current team).
• Ethiopia Premier League
St. George FC (2003 -2004)
•CAF Champions League
St George FC, Ethiopia (2003-2004)
• CAF Confederation Cup
Ashanti Goldfields SC, Ghana (1999-2000)
• Football Academies
Red Bull Academy 2007 – 2008)
Feyenoord Academy (2009 – 2010)

QUALIFICATION AND COMPETENCY DETAILS
 • UEFA  License A. - Certificate Team building. - CAF License B. 
• Fluent in Dutch and English
• Experienced with different cultures and religions 

ACHIEVEMENT AND AWARD DETAILS
Total Career: 500+ matches for FC Den Bosch in the Dutch National League
League Cup Final (1993 – 1994) – FC Den Bosch
Promotion to Dutch Premier League (1994-1995) – FC Den Bosch
Promotion to the Ghana Premier League (2002 – 2003) – Heart of Lions FC
Ethiopian Super Cup Winner (2004 – 2005) – St George FC
CAF Champions League Qualification (2004 – 2005) – St George FC, Ethiopia
Two-time Qualifier – CAF Confederation Cup (1998 – 2001) – Goldfields SC, Ghana
CAF Champions League Qualification (2006 – 2007) – Heart of Lions FC, Ghana
Runners Up – GHALCA Top Four Competition (2006 – 2007) – Heart of Lions FC, Ghana
Awarded Best Coach in Ghana Premier League (2006 – 2007)
Awarded Honourary Membership (1992) – FC Den Bosch
Enzo Ferrari International Youth (Under-18) Tournament Winner in Modena, Italy (1998) – with Shizuoka FC, Japan
Runners-Up - International Under-17 Tournament for Professional Teams in Tiel, Netherlands 2009) – Feyenoord Academy, Ghana
Winners - International Under-17 Tournament for Professional Teams in Groesbeek, Holland (2009) – Feyenoord Academy, Ghana
Loyalty and Sportsmanship Award by the Dutch Football Association for Silver Jubilee (25 years) with FC Den Bosch, Holland
Supporters Player of the year Award – FC Den Bosch, Holland

Recent Coaching Details
Winners – President’s Cup (Ghana), June 2012 (with Berekum Chelsea FC)
Ongoing campaign in the final group stages (Money Zone) of the 2011/2012 CAF Champions League with Berekum Chelsea FC  [Group B with Al-Ahly (Egypt),
       Zamalek (Egypt) and TP Mazembe (DR Congo)].

5 comments:

  1. Misifa. Kibao!
    Muda c mrefu atakuwa flop.

    ReplyDelete
  2. Karibu kocha mpya lkn kwa soka la bongo, kocha mlango aliouingilia ndio atakaoutokea

    ReplyDelete
  3. mimi naona hatodumu akifungwa na simba kazi hana shafii ww yanga au simba maana skusomi

    ReplyDelete
  4. Mazzingira ya kumwondosha Brandts yananiaminisha hata akija morinyo atatimuliwa siku si nyingi. Hebu fikiria kocha anaondolewa coz timu haijapata ushindi mechi ya simba? Ni wazi kamwe soka halitapiga hatua hata siku moja kama mtazamo huu hautabadilika.

    ReplyDelete
  5. Mazzingira ya kumwondosha Brandts yananiaminisha hata akija morinyo atatimuliwa siku si nyingi. Hebu fikiria kocha anaondolewa coz timu haijapata ushindi mechi ya simba? Ni wazi kamwe soka halitapiga hatua hata siku moja kama mtazamo huu hautabadilika.

    ReplyDelete