Search This Blog

Wednesday, January 1, 2014

DIEGO COSTA: RONALDO NDIO ANASTAHILI KUTWAA BALLON D'OR

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa amesema angependelea tuzo ya Ballon d'Or iende kwa Cristiano Ronaldo mwaka huu.

Ushindani wa tuzo hiyo mwaka huu ni mkubwa sana, huku mshambuliaji huyo wa Real Madrid na Ureno - ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka 2008 - anaungana na mshindi wa mara 4 wa tuzo hiyo Lionel Messi na Frank Ribery.

Baadhi ya wanamichezo wakubwa duniani wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu nani anayestahili kushinda tuzo hiyo, huku mshindi akitangazwa mwezi ujao tarehe 13.

Akiongea kabla ya mchezo wa hisani wa 'Champions for Life' katika uwanja wa Santiago Bernabeu jana jumatatu, mwandishi wa habari alimuuliza Costa chaguo lake baina ya washindani wa watatu wa Ballon d'or, na mshambuliaji huyo akajibu: "Cristiano."

2 comments: