Search This Blog

Wednesday, January 8, 2014

BAADA YA KIPIGO CHA JANA - MOYES AKANUSHA TAARIFA ZA KUMSAINI FABIO COENTRAO


Kocha wa Manchester United David Moyes amekanusha taarifa kwamba klabu hiyo ipo mbioni kumsaini beki wa kushoto wa Real Madrid Fabio Coentrao.

Ripoti zilizosambaa katika vyombo vya habari vya barani ulaya zinasema kamba United na Madrid zimekubaliana bei juu ya beki huyo mwenye 25 kutoka Ureno ili aweze kujiunga na klabu ya  Old Trafford.

Lakini akiongea jana usiku baada ya kipigo cha 2-1 dhidi ya Sunderland katika nusu fainali ya Capital One Cup kwenye dimba la Stadium of Light, Moyes alikanusha taarifa hizo. 

"Hapana, sio ukweli," alisisitiza kocha huyo wa kiscotland ambaye jana iliripotiwa amepewa kiasi kisichopungua paundi millioni 200 kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake chenye hali mbaya. 

1 comment: