Search This Blog

Monday, December 30, 2013

TFF KUWENI MAKINI NA MAAMUZI YA BODI YA LIGI, KAMA KWELI TUNATAKA MAENDELEO YA SOKA TUACHANE NA SIASA....


KANUNI YA 24
KUVURUGA MCHEZO
1.     Wachezaji na viongozi wa timu itakayosababisha mchezo kuvurugika na hatimaye kuvunjwa, itapoteza mchezo huo hata kama ilikuwa inaongoza kwa magoli na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu, iwapo timu pinzani inaongoza kwa magoli zaidi ya matatu, itabakia na idadi ya magoli hayo iliyokwishafunga.

2.     Magoli yaliyofungwa na wachezaji wa timu iliyosababisha mchezo kuvunjika yatafutwa lakini magoli yaliyofungwa na timu pinzani hayatofutwa na yataendelea kuonekana katika idadi ya magoli yaliyofungwa na wachezaji wa timu hiyo wakati wa kutafuta mfungaji bora.

3.     Endapo itatokea vurugu ya aina yoyote ile na kusababisha mchezo kusimama, mwamuzi atasubiri kwa dakika zisizozidi kumi na tano, na endapo hali ya vurugu bado inaendelea mwamuzi atavunja mchezo na kuwasilisha taarifa ya mchezo kwa kamati ya Usimamizi ya ngazi husika.

4.     Timu iliyosababisha vurugu itapoteza mapato yote ya mchezo.

5.     Timu iliyosababisha kuvurugika kwa mchezo italipa faini ya shilingi 300,000/=.

3.           Faini hiyo italipwa kabla ya mchezo unaofuatia.

4.           Mchezaji/wachezaji na kiongozi/viongozi watakao bainika kusababisha vurugu zilizopelekea mchezo huo kuvunjika watafungiwa kujihusiha namasuala yote ya mpira kwa kipindi cha miaka mitano.

5.           Endapo uvunjikaji wa mchezo utakuwa nje ya kanuni ya 22(3), mchezo huo utarudiwa kama inavyoainishwa katika kanuni ya 9(e) na utachezeshwa na waamuzi wengine katika siku itakayo pangwa na chombo husika. 


2 comments:

  1. Hi Shaffi, kwanza nikupongeze kwa hili. binafsi niliiyona hiyo clip kwenye local tv mmoja ya hapa nchi last week. niliamua kutuma messgae kwenye kipindi chenu bora kabisa cha michezo cha sports extra, unfortunately hiukusomwa. Shaffi, hao TFF waache ubabaishaji, its clearly seen on that clip JKT ndiyo walikuwa wameanzisha hizo vurugu, refa ikabidi naye ajitetee kama binadamu. sasa hili swala la mechi kurudiwa linatoka wapi? tena hao walionzisha vurugu wanaonekana waziwazi kwanini wasichukuliwa hatua, Jeuri hiyo wameleta kwakuwa wao ni JTK je wangekuwa JWTZ si wangeua kabisaa. Mwisho nikupongeze wewe wa team yako nzima kwanye kwa kufichuwa uozo uliokuwepo kwanye michezo, keep it up....tupo pamoja, Happy new year. Ray

    ReplyDelete