Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji.
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.
Maneno ya mkosaji,Bonanza mbona mlipelek timu yenye hadhi ya hali ya juu ?inakuaje timu yenye hadhi ya juu kucheza bonanza? Unaweza ukawa na pesa lkn ukawa huna furahaa kwa stress ,Simba hawajapata hela lkn wanafurah na wameweka historia yanga walopata hela wamebaki kuwa cha mdoli
ReplyDeletehela ndio kilakitu wewe acha kelele
DeleteHizobhela ambazo ndo kila kitu wewe kajamba nani wapata ngapi? Wewe furaha yako ni ushindi wala hufaidiki na chochote ktk hizo hela mashabiki tunafurahia ushindi na wala c pesa
DeleteKama ni bonanza, kulikuwa na haja gani ya kumchezesha Okwi aliyefanya mazoezi siku moja tu? Je, hiyo sio baada ya kuzidiwa na kukosa wachezaji mbadala? Kama mchezo haukuwa na umuhimu, kwa nini wasipangwe wachezaji waliokuwa kambini na kocha kwa muda mrefu ingawa viwango vyao ni vya chini kidogo kulinganisha na mapro waliofika kambini muda mfupi kabla ya mechi? Tangu lini Manji akaangalia mapato ya hela mbele ya matokeo ya mchezo?
ReplyDeleteNa mashabiki siku zote tunahitaji ushindi wa magoli. Hela hazileti raha yoyote kwa mashabiki. Manji akubali tu walizidiwa mbinu za kiufundi.
ReplyDeleteNdio maana amewapongeza simba kwa mchezo mzuri na ushindi,ukiangalia ni kweli yanga ndio wamefaidika zaidi kwakupata hela kwani kilichokuwa kinashindaniwa ni pesa na wala sio pointi wala nini, nyie kaeni na ushindi wenu bila pointi na sisi na mijihela yetu. yanga mbele daima.
ReplyDeletekweli mnajisahaulisha, mmesahau makubaliano ya mechi ilikuwa kuchezesha vikosi vya kwanza? Wanasimba acheni ujinga uliopitiliza lile ni bonanza
ReplyDeleteKuna kabila moja wanawake wake wanawema afadhali kulia kwenye benz kuliko kucheka kwenye baiskeli, simba wanacheka kwenye baiskeli mvua jua taabu tupu. Ngojeni round ya pili mtatafutana mana hata uwanjani mlishaanza kususia kuja kwa match ya jana mtajazana match ya marudiano na mtasambalitika na hiyo baiskeli yenu. Hongera chairman hiyo ilikuwa bonanza tuu na huyo Akilimali tukiongeza hana akili wa mali ni mjinga na mbumbumbu wa kupitiliza kutwa kuzungumzia uchawi si aisadie taifa stars ichukue hata kombe la dunia
ReplyDeleteHapo manji umenena coz mpira ni pesa ndo maana wenzetu wana tawi la mpira pesa..
ReplyDeleteKwa hiyo kikosi cha kwanza cha yanga hakina uwezo mbele ya mnyama ndo mana kimetandikwa?
ReplyDeleteWALEVI WAKUBWA NYIE!
ReplyDeleteKAMA NI KULOGOTA VIZIBO MNATSHA NA BADO KWA SIMBA MTALOGOTA SANA MIPIRA MU NYAVU!
kama hamtaki ushindi mnataka pesa si mfungue duka la kamdambili jangwani.
KUFUNGWA NA MTANI NI ZAIDI YA MILIONI MIA. WATU WANSZIMIA NS HADI KUFA' wengine wameweka wake zao rehani!
ETI BONANZA!
NA KOCHA MBONA MNAMLA KICHWA?
Maneno ya mkosaji, na hekaya za 'sizitaki mbichi hizi'. Imewauma hadi mnalaumiana kuhusu kaseja. Ngasa alilia kabisa, mmepigwa tu
ReplyDeleteSawa ni bonanza lkn tumewachapa kwa hilo bonanza pamoja na mastaa wenu wenu wote wa jangwani,
ReplyDeleteKipigo ni kipigo tuu tuache kelele bhanaa.sawa bonanza kwa hyo mnasema baada ya kufungwa kipindi mnatambiana mtaani mulikuwa hamyajui hayo kama ni bonanza.na hyo manji mbona hakufafanua toka mwanzo...ndio nyie mnataka dem akikutosa mnasema malaya tuache vsingizio.... hapohapo bona mbona
ReplyDeleteBonanza lamfukuza kocha jangwani wewe umeona wapi mtu akaitwa embe? Manji kwa lugha ya kiarabu ni embe, mheshimiwa embe amfukuza kocha kwa sababu ya bonanza wala c sababu ya kiwango kwani hamkukion kikosi chenu dhidi ya kmkm mbona hamkumtimua ? Mnyama ameleta balaa jangwani
ReplyDeletekwani katika bonanza kunahitaji mazoezi?ndio maana okwi akacheza.Simba walipania mno mechi hii ili wamalize mgogoro na kulipiza machungu ya Okwi kusajili Yanga,ndio maana wakaingia gharama ya kuweka kambi zanzibar kwa ajili ya mechi moja tu ya bonanza.mtaendelea kubeba makombe ya mbuzi tu .Haya ndio mashindano yenu makubwa mnayoshiriki wakati yanga mwakani wana mashindano ya klabu bingwa africa na kagame.Hongereni kwa ushindi wa bonanza na kombe la mbuzi sisi ndio kwanza tunaingia kambini uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya maana
ReplyDeleteMTASEMA MENGI KISHABIKI LAKUNI 3-1 ZIPO PALE PALE TANGU LINI MANJI AKAPENDA PESA KULIKO USHINDI SIZITAKI MBICHI HIZI
ReplyDeleteKwani ni mara ya kwanza kwenda uturuki ? Mtakwenda mtarudi mtaidhia hivy hivy kutandikwa hakuna jipya mtakalolileta sisi mkishawatoa vibonde wakomoro mtaishia kwa waarabu walee walowapiga nne kipindi kile
ReplyDeleteMwanaume unaliwa kiboga unasema nilikuwa nimelewa mmekula kiboga pombe! kweli nyie Yanga mashoga!
ReplyDelete