Search This Blog

Tuesday, December 17, 2013

MAGOLIKIPA WA LIGI KUU KUKIPIGA NA CLOUDS MEDIA BOXING DAY.


 Shabani Kado akiwa na baadhi ya wachezaji wa Clouds, Jeff Lea ( kushoto ),Shaffih Dauda ( katikati ) na Mbwiga Mbwiguke.

Timu ya magolikipa wa vilabu vya ligi kuu ya Vodacom wanataraji kukipiga na timu ya wafanyakazi wa CLOUDS MEDIA siku ya tarehe 26/12/2013 ( Boxing Day ) kwenye uwanja wa KINESI uliopo maeneo ya Ubungo.
Nahodha wa timu ya magolikipa Shabani Kado amesema timu yao itawaonyesha mashabiki uwezo mkubwa wa kucheza ndani,'' siku iyo sisi magolikipa wote tutacheza ndani na golini itabidi wadake wengine ambao wamezoeleka kucheza ndani''
Mara nyingi mashabiki wetu wanadhani hatuna uwezo wa kucheza ndani,mfano sidhani kama watanzania wanajua Juma Kaseja ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya ushambuliaji ukiachilia nafasi yake aliyozoeleka ya kukaa langoni,sasa siku iyo ndio watatuona moto wetu,
kwa upande wa timu ya CLOUDS nahodha wa timu hiyo MBWIGA MBWIGUKE 'KISHETI' yeye amesema timu yao ipo gado na kuelekea mchezo huo watacheza mchezo wa kirafiki na mashabiki wa YANGA siku ya IJUMAA ya tarehe 20/12/2013 kwenye Dimba la Tanganyika Packers.


No comments:

Post a Comment