Guus Hiddink amesaini mkataba wa miaka minne na timu ya taifa ya Uholanzi.
Kocha huyo wa kidachi amekubali kuchukua majukumu ya kocha sasa wa timu hiyo ya taifa Louis van Gaal baada ya fainali za kombe la dunia mwaka 2014 kwa miaka miwili kama kocha, na kufuatiwa na miaka mingine miwili kama mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo ya taifa.
Haitegemewi kwa Hiddink kutambulishwa na FA ya Uholanzi mpaka mwaka mpya lakini vyanzo vya kuaminika vinasema kwamba kila kitu kipo tayari kwa ajili ya kutangazwa.
Hiddink, ambaye aliiongoza Uholanzi kutoka mwaka 1994-1998, alizungumza hivi karibuni matamanio yake ya kurudi kuifundisha timu hiyo kwa mara ya pili.
Kocha huyo mwenye miaka 67 alikuwa nje ya soka kwa muda mrefu kiasi tangu alipojiuzulu kuifundisha Anzhi Makhachkala mwezi July 2013.
Hiddink ana uzoefu mzuri kwenye michezo ya kimataifa akiwa tayari ameshaviongoza vikosi vya Russia, Australia, South Korea na Turkey pamoja na nchi yake ya Uholanzi.
No comments:
Post a Comment