Search This Blog

Thursday, December 5, 2013

BREAKING NEWS….! MCHEZAJI BORA UHAI CUP HANA MKATABA YANGA, KLABU KUBWA NCHINI KUMSAJILI MUDA WOWOTE KUANZIA SASA….!


MCHEZAJI Issa Ngao wa kikosi cha Yanga chini ya miaka 20 (U20), muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa miaka minne kuichezea moja ya klabu kubwa hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa zilizoufikia mtandao huu, Ngao hadi anaichezea Yanga katika michuano ya Kombe la Uhai mwaka huu, hakuwa na mkataba wa kuitumia Yanga hivyo habanwi na hali yoyote ile kuachana na klabu hiyo.

 

Kiongozi mmoja wa klabu kubwa ambayo ipo katika hatua za mwisho za kumsajili mchezaji alisema; “Kabla ya kumfuatilia tulichunguza kujua kama ana mkataba na Yanga au la, tumejua hana mkataba hivyo zoezi letu la usajili halitakuwa gumu na muda wowote tutakamilisha kila kitu.” 

Mtandao huu uliporudi kwa mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye awali alikataa kuzungumzia mambo ya timu ya vijana hadi alipohakikishiwa kuhifadhiwa jina lake alisema; “Huyu kijana kweli hana mkataba na Yanga na anacheza tu kienyeji, sasa kama kuna watu wanasema wanamsajili sawa, lakini tutapata pigo.”

Ngao alifanya vizuri katika michuano ya Kombe la Uhai ambayo hushirikisha vikosi vya U20 vya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara licha ya Yanga kushika nafasi ya pili baada ya kufungwa na Coastal Union katika fainali.

3 comments:

  1. ushabiki huo shafii dauda

    ReplyDelete
  2. Waache wamsajili lakini kumbuka nyumbani ni nyumbani, atarudi tu na kuwaachia maumivu hao wanaomshadia! Au wamesahau ya Ngasa?

    ReplyDelete
  3. Huyo dogo anajua mbaya ni bonge la kitasa yanga tutajuta huwa hana papara kabisa

    ReplyDelete