Search This Blog

Tuesday, November 12, 2013

STEWART HALL NA UJUZI WAKE, AZAM NA SIASA ZA SOKA LA BONGO...KOCHA Stewart Hall aliyachana na Azam FC amesema ilikuwa lazima aachane na klabu hiyo kutokana na mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yasingeweza kumfanya aendelee kuifundisha timu hiyo kwa siku nyingine.


Katika mahojiano maalum na kocha huyo yaliyofanywa muda mfupi baada ya kubwaga manyanga ya kuifundisha Azam, Hall anasisitiza kwamba hana kinyongo na mfanyakazi yeyote wa Azam. Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo:

  Ilikuaje hadi ukaamua kuachana na Azam?
Nadhani muda ulikuwa umeshafika wa mimi kufanya hivyo kutokana na siasa za timu ile lakini pia kuna kazi nyingine ambayo ilikuwa imekuja mbele yangu hivyo nisingeweza kuachana nayo.
 
Majukumu yako ya msingi kabisa wakati unajinga na Azam yalikuwa ni yapi?
Niliwambia viongozi kama kweli walikuwa wanataka kuuvunja ufalme wa Simba na Yanga isingewezekana kuwa kazi nyepesi,ilitakiwa kwanza kuhakikisha wanakaa katikati ya hizi timu mbili,kila mwaka kati ya Simba na Yanga mmoja wao anakuwa dhaifu na mwingine anakuwa na nguvu kwaiyo njia pekee ilikuwa ni kuhakikisha tunakuwa juu ya yule dhaifu,tatizo la timu hizi ni siasa na ugmvi baina ya viongozi wao kitu ambacho hupelekea kuwapa ajira makocha na kusajili wachezaji wabovu,sasa kuna mwaka unaweza kuiona Yanga ipo bora huku Simba ikiwa inalegalega siku zinazofuata mambo yanabadilika, Simba inaweza kuwa imara halafu Yanga inakosa nguvu sasa unapozungumza ubingwa ni lazima kwanza uhakikishee unakaa katikati ya hizi timu mbili kongwe.  Umesema siasa zimekufanya uondoke Azam, unaweza kutuambia ni siasa za aina zipi hizo? 
  Ni nyingi lakini ngoja nikutajie moja ya maana ambayo unaweza kuiona, unakuta tumeweka mipango kadhaa ya maana kuhusu maendeleo ya timu lakini ajabu timu ikipoteza mechi moja tu kila kitu kinakufa katika ile mipango ya kukuza timu tuliyojiwekea. Halafu kuna kitu kinaitwa kuiacha timu nje, kuna wakati nakuta wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza ni wagonjwa nami kuwa kutambua hilo nalazimika kuwaacha benchi, ukifanya hivyo ni tatizo wanakuja watu kukuambia eti timu yote naiacha benchi makusudi. Kuna mechi moja  wachezaji kadhaa kama Bocco (John), Kipre Tchetche, Sure Boy (Salum Aboubakari) na Hunfrey Mieno wote walikuwa wagonjwa nami nikawaacha benchi sasa baada ya kufanywa hivyo nikaulizwa kwa nini naiacha benchi timu nzima, sikuwaelewa lakini nikaanza kuhisi kuna jambo linaloendelea.

  Unadhani kwa nini Azam hawakuwa wakifuatilia rekodi yako na badala yake wakaendeleza mambo ya siasa?
Mimi nadhani wenyewe ndiyo walikuwa na matatizo ya kushindwa kufahamu kama mimi nafanya kitu gani na wao wanatakiwa kufanya kipi, tazama timu ipo nafasi ya pili tena kwa tofauti ya pointi moja tu, halafu bado naonekana sifahi na mambo mengi nafanyiwa sasa nifanyeje?

  Umejifunza  nini kwa yote yaliyokukuta Azam?
Nilichojifunza ni kwamba soka la Afrika limetawaliwa na viongozi ambao ni wanasiasa kuliko hali halisi ilivyo, tazama wameniambia timu haina mwelekeo huku wakisahau kwamba Azam imecheza mechi sita nje ya Dar es Salaam huku Simba na Yanga zikicheza mechi mbili nje ya Dar es Salaam, hakuna asiyejua ugumu wa mechi za nje ya Dar es Salaam. Kwa bahati nzuri hatukufungwa hata mechi moja, sasa ubaya wangu unatokea wapi kwa kutazama uwiano huu? Ngoja nikueleze ukweli, kwa kweli mikoani viwanja vingi ni vibaya na tukiwa huko tunalazimika kucheza soka la juu kwa juu bila kuweka mpira chini kitu ambacho si asili yetu, na hili tucheze vizuri huwa tunalazimika kucheza soka la chini kwenye uwanja wetu wa Chamazi au Taifa lakini kwingine kote hali ni ngumu.


  Unadhani kuondoka kwako hakutawaathiri wachezaji?
 Sidhani kwani nimewajenga kisaikolojia kujua namna kuishi bila mimi maana mimi ni mwanadamu na lolote laweza kutokea.

Unadhani kitu kipi kilikuathiri na kupata matokeo ya kusuasua?
Kwanza ni majeruhi na jambo lingine ni idadi ya majeruhi katika kikosi cha kwanza.

Ukiwa Azam ni changamoto zipi ulizokutana nazo kutoka kwa wachezaji?
Tatizo kubwa ni wachezaji wengi kukosa msingi wa soka, mchezaji mwenye umri wa miaka 21 unaanza kumfundisha misingi ya soka ambayo Ulaya anafundishwa mtoto wa miaka 7 hadi 11, sasa kwa hali hiyo usitegemee kumpata mchezaji mzuri haraka.


Umesema kwamba, umepata timu mpya ya kufundisha unaweza kutuambia ni timu gani hiyo?
Ahaaah..... aeheeeeeee......, nadhani ngoja nikueleze ukweli lakini siku zitatuambia zaidi.
USIKOSE SEHEMU YA PILI YA MAHOJIANO HAYA.

No comments:

Post a Comment