Search This Blog

Wednesday, November 6, 2013

SD TV: MWAMUZI ALIYEPIGWA KWENYE MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA KATI YA STAND UTD Vs JKT KANEMBWA. NINI MAONI YAKO ?

3 comments:

  1. Nasubiri kuona uongozi mpya utafanya nini maana wakati Rais mpya anakabidhiwa ofis Bw Jamal Malinzi aliahidi kushughulikia vitendo hivi kwa nguvu zake zote.
    nanukuu,
    niongelee suala la fujo viwanjani. Mpira ni dakika tisini. Katika kipindi hicho uamuzi wa mwamuzi unakuwa ni wa mwisho. Tusifiche upungufu wa timu zetu kwa kujificha nyuma ya kivuli cha mwamuzi. Waamuzi wakionekana wamefanya makosa yawe ya makusudi au ya bahati mbaya vyombo vya kuwahukumu vipo, mahakama ya waamuzi sio mashabiki. Kitendo cha mashabiki kufanya fujo kabla, wakati na baada ya mechi ya mpira kamwe hakikubaliki mahali popote duniani. Kanuni za FIFA, CAF na TFF ziko wazi na adhabu zinajulikana. Moja ya adhabu hizi ni timu husika kucheza kwenye uwanja mtupu usio na mashabiki kama ilivyowatokea Al Ahly na Zamalek huko Misri au kucheza nje ya uwanja wako kama ilivyowatokea Senegal ambao baada ya vurugu Dakar, Senegal waliamriwa na FIFA mechi zao za nyumbani wachezee nje ya nchi na wakachagua kuchezea Morocco.
    Ndugu zangu yaliyotokea majuzi Mbeya na Dar es salaam wote tumeyasikia na wengine miongoni mwetu hapa ni mashuhuda. Ninasema iwe mara ya kwanza na y a mwisho. Kwenye masuala ya kutekeleza mahitaji ya kanuni uongozi wangu hautaionea haya klabu yoyote, iwe mpya au kongwe kwenye ligi yetu. Ni jukumu la viongozi wa klabu kudhibiti wanachama na wapenzi wao. Tabia ya benchi la ufundi kutoa matamshi yanayoweza kuamsha hisia za mashabiki ni kinyume na taratibu na kanuni ziko wazi kuhusu jambo hili. Viongozi wa klabu na mabenchi yao ya ufundi wakishindwa kutekeleza wajibu wao tusilaumiane.

    ReplyDelete
  2. niongelee suala la fujo viwanjani. Mpira ni dakika tisini. Katika kipindi hicho uamuzi wa mwamuzi unakuwa ni wa mwisho. Tusifiche upungufu wa timu zetu kwa kujificha nyuma ya kivuli cha mwamuzi. Waamuzi wakionekana wamefanya makosa yawe ya makusudi au ya bahati mbaya vyombo vya kuwahukumu vipo, mahakama ya waamuzi sio mashabiki. Kitendo cha mashabiki kufanya fujo kabla, wakati na baada ya mechi ya mpira kamwe hakikubaliki mahali popote duniani. Kanuni za FIFA, CAF na TFF ziko wazi na adhabu zinajulikana. Moja ya adhabu hizi ni timu husika kucheza kwenye uwanja mtupu usio na mashabiki kama ilivyowatokea Al Ahly na Zamalek huko Misri au kucheza nje ya uwanja wako kama ilivyowatokea Senegal ambao baada ya vurugu Dakar, Senegal waliamriwa na FIFA mechi zao za nyumbani wachezee nje ya nchi na wakachagua kuchezea Morocco.
    Ndugu zangu yaliyotokea majuzi Mbeya na Dar es salaam wote tumeyasikia na wengine miongoni mwetu hapa ni mashuhuda. Ninasema iwe mara ya kwanza na y a mwisho. Kwenye masuala ya kutekeleza mahitaji ya kanuni uongozi wangu hautaionea haya klabu yoyote, iwe mpya au kongwe kwenye ligi yetu. Ni jukumu la viongozi wa klabu kudhibiti wanachama na wapenzi wao. Tabia ya benchi la ufundi kutoa matamshi yanayoweza kuamsha hisia za mashabiki ni kinyume na taratibu na kanuni ziko wazi kuhusu jambo hili. Viongozi wa klabu na mabenchi yao ya ufundi wakishindwa kutekeleza wajibu wao tusilaumiane.

    ReplyDelete
  3. mimi nasema hivi hawa waamuzi ndio waotia hasira watu.mchezaji anashika mpira mara ya kwanza unapeta ya pili unapeta mwishowe wanona sawa tu kwani wanajua wewe wao .chapa hawa waamuzi washike adabu

    ReplyDelete