Search This Blog

Friday, November 15, 2013

RONALDO VS ZLATAN: JOHAN CRUYFF ATAJA ANAYETAKA AMUONE AKIFUZU KWENDA KOMBE LA DUNIA

Gwiji wa soka wa Uholanzi Johan Cruyff angependa kuona  Cristiano Ronaldo akienda kucheza kombe la dunia 2014 mbele ya   Zlatan Ibrahimovic.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona amesema kwamba ni jambo baya kuona aidha Ronaldo au Ibrahimovic wakikosa nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa ya dunia, lakini angependa zaidi kumuona staa wa Ureno Cristiano Ronaldo akifuzu na timu yake mbele ya Sweden ya akina Ibrahimovic.

"Ni jambo baya kwa kombe la dunia kwamba mmoja kati  ya washambuliaji bora duniani hatoweza kucheza michuano hiyo. Ni ni jambo la kuhuzunisha," Cruyff aliiambia Algemeen Dagblad.

"Sina yoyote ninayempendelea kati ya hawa wawili, lakini nikitakiwa kuchagua mmoja kati yao yupi  ningependa kumuona akiingia World Cup na timu yake, basi ningependa kumuona Ronaldo akifuzu." 

5 comments:

  1. safi sanaaaa cr7 nampigia njema duwa

    ReplyDelete
  2. cR7 Ajitaidi naye aende Brazilian

    ReplyDelete
  3. Nataka kushuudia cr7 akichiriki combe la dunia bhanaaaaaa

    ReplyDelete
  4. Cr7 anatisha mechi 17 magori 24 klabu bingwa,magori 16 lariga,amefunga jumla ya magori 68 ktk mashindano yote ya mwaka huu

    ReplyDelete