Search This Blog

Thursday, November 14, 2013

MIMI NI SHABIKI WA LIVERPOOL,KAMA NISINGEKUWA BONDIA NINGEKUWA GOLIKIPA- FRANCIS CHEKA

Jina langu ni Francis Boniface Cheka, mimi ni mshabiki wa Liverpool.
 Swali: Lini ulianza kuishabikia Liverpool?
 Cheka: Nakumbuka nilianza kuipenda Liverpool mwaka 2002  na kipindi hicho ni mchezaji Michael Owen ndiye aliyenihamasisha kwa jinsi alivyokuwa anafunga.

Swali: Ni siku gani uliyofurahi kuliko zote kama mshabiki wa Liverpool?

Cheka: Siku niliyofurahi kuliko siku zote nikiwa mshabiki wa Liverpool ilikuwa ni mwaka 2005 wakati liverpool ilipochukua klabu bingwa ya Ulaya kwa kuifunga AC Milan.

Swali: Unafikiri matatizo yanayoikumba Liverpool kwa sasa yamesababishwa na nini?

Cheka: Matatizo kwenye timu yanatokea pale ambapo watu wanakuwa hawatimizi wajibu wao kwenye timu, nadhani hilo ndio linaloikuta Liverpool kwa sasa, pia kuna baadhi ya wachezaji ambao hawatimizi wajibu wao nafikiri hayo ndio yanayoiathiri timu.

Swali: Na je ni nini kinapaswa kufanywa ili kuinusuru timu yako?

Cheka: Nadhani wachezaji wanapaswa kuwa na juhudi za dhati za kuiokoa timu kwa kuwa nadhani wao ndio wenye wajibu na uwezo mkubwa wa kufanya hivyo. Kocha atafanya kazi yake atafundisha atamaliza asilimia inayobaki ni kwa wachezaji.

Swali:  Na hapa nyumbani wewe ni shabiki wa timu gani?

Cheka: Hapa mimi nashabikia Simba lakini baba yangu mzazi Mzee Cheka ni Yanga damu nakumbuka kuna siku Simba iliifunga Yanga bao nne mzee alinichapa baada ya kumcheka na timu yake.

Swali: Je, kuna uhusiano wowote na upenzi wako kwa Simba na bukta za rangi nyekundu na nyeupe unazovaa ukiwa ulingoni?

Cheka: Hapana, unajua mimi nampenda sana Mohamed Ali na yeye ndio alinivutia mpaka mimi kuvaa kama yeye, kwani nilidhani kuwa ili bondia apigane vyema kama Mohamed Ali ni lazima avae kama yeye.

Swali: Wakati unacheza soka ulikuwa ukicheza nafasi ipi na uliwahi kucheza timu gani?

Cheka:  Mimi  nilikuwa golikipa, nimeshacheza timu kama FC Nondo, Shoka FC, Care Boys na nyingine ya Msumbiji ya Sportive De Moeda pamoja na Kilimani Benfica ambayo ilikuwa ligi daraja la nne Msumbiji. Nakumbuka wakati nadakia Care Boys kuna mchezaji mmoja Marehemu James Shawa aliwahi kunitegua kidole kwa shuti lake.

Swali: Baada ya kuumia kwenye soka ndio ukaamua kuingia kwenye ndondi au?

Cheka: Hapana, niliingia kwenye ndondi kwa kuwa nilikosa nafasi kwenye soka, nakumbuka baba yangu aliwahi kunipeleka Yanga mwaka 1997 wakati huo usajili ulikuwa wazi kwa watu wote, aliponipeleka nilikataliwa na ndio ikabidi anipeleke kwenye ndondi.

Swali: Ni wachezaji gani watatu ambao siku zote wako kichwani mwako?

Cheka: Nizar Khalfan, Juma Kasseja na Mussa Hassan Mgossi na kwa Liverpool ni Steven Gerald.

No comments:

Post a Comment