Search This Blog

Sunday, November 3, 2013

KAMPENI YA NANI MTANI JEMBE ILIVYOFANA WILAYANI KINONDONI.

 Wasanii wa kundi la Wakali Dansi la jijini Dar es Salaam likiwaburudisha mashabiki wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager katika kampeni ya Nani Mtani Jembe iliyofanyika Kinondoni Manyanya jana . Kampeni hiyo ni maalum kwa mashabiki wa Simba na Yanga
 Mashabiki wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakiwa wananunua Bia hiyo ili kujishindia zawadi zilizokuwa zinatolewa katika kampeni ya Nani Mtani Jembe iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Mshereheshaji katika kampeni ya Nani Mtani Jembe (kulia) akimkabidhi zawadi ya jezi Mshabiki wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayoendesha kampeni hiyo kwa ajili ya mashabiki wa Simba na Yanga iliyofanyika Kinondoni kwa Manyanya Dar es Salaam jana.


 Mtoa huduma katika kampeni ya Nani Mtani Jembe, Mwanahamisi Selemani wapili (kulia) akizungumza na mashabiki wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayodhamini Timu za Simba na Yanga iliyofanyika Kinondoni Dar es Salaam jana.
 Mohamed Bakary (kushoto) ambaye ni mshereheshaji katika kampeni ya Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na Bia ya Kilimanjaro akizungumza na mmoja wa shabiki wa bia hiyo katika kampeni iliyofanyika Dar es Salaam jana maalum kwa mashabiki wa Simba na Yanga.
 Mtoa huduma katika  kampeni ya Nani Mtani Jembe, Mwanahamisi Selemani (kulia) akimkabidhi zawadi ya Jezi shabiki wa Bia ya Kilimanjaro na timu ya Yanga katika kampeni hiyo iliyofanyika Kinondoni Dar es Salaam jana.
 Mashabiki wa Timu ya Yanga na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakiwa juu ya jukwaa wakishindana kupuliza Vuvuzela katika Promosheni ya Nani Mtani Jembe iliyofanyika Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment