Search This Blog

Monday, October 28, 2013

WACHEZAJI WA KASSA MUSA NA GEORGE MASATU WATEMBELEA KABURI LA MAREHEMU IDRISSA NGULUNGU

 Mchezaji wa Zamani   George Masatu Aliyetembelea Kaburi la Mchezaji wa Zamani Marehemu Idrissa Ngulungu
Kiungo wa zamani wa Coastal Union kassa Mussa amefunga safari  kuja mkoani Morogoro Kuzuru kaburi la rafiki yake kipenzi ldrissa Kulungu aliyefariki kwenye ajari ya gari Agost 1 mwaka huu Katika ajari hiyo ldrisa Ngulungu na mtoto wa dada yake Leila Kapilima walipoteza maisha papo hapo huku baadhi ya wanafamilia wa ukoo huo wa ngulungu walijeruhiwa vibaya.
 Mbali na kassa Mussa mchezaji Aliambatanana Mchezaji wa zamani George 
Akizungumza kwenye makaburi hayo ya Kolla baada ya shughuli ya kuwasomea Dua marehemu hao Kassa Mussa Mussa alisema kwamba akiwa Ulaya alilia sana baada ya kupata taarifa ya kifo cha ghafla cha rafiki yake huyo.
" Kiukweli nililia sana baada ya kupokea taarifa za kifo cha rafiki yangu kipenzi ambaye tulikuwa tukiwasiliana kwa simu kila baada ya siku tatu,juzi nimetoka Ulaya kuja hapa Morogoro kwa lengo moja tu la kuzuru kaburi la rafiki yangu"alisema Kassa Mussa na kuongeza kusema
Mimi na ldrisa ni miongoni mwa wachezaji tuliopia ubingwa Coastal Union Mwaka 1988 ldrissa akicheza namba 4,Kaumba akicheza 6 na mimi nikicheza namba 8"alisema Kassa Mussa na kuangua kilio huku akiendela kurekodiliwa na kamera za za mtandao huu. ambapo Beki wa zamni wa Reli ya Morogoro
 Mohamed Mtoni alibeba jukumu la kumbembeleza Kassa Mussa ambapo aliponyamza Mtandao huu ulibadili maswari na kumtaka azungumzie soka la sasa hapa nchini ambapo pamoja na mambo mengine kiungo huyo wa zamani alimponda mchezaji wa simba Ramadhan Singano kupewa jina la Messi habari hiyo itawajia hivi punde
 Husein Ngulungu,kaka wa ldrissa Ngulungu
     Kassa Mussa aliyeambatana na George Masatu walipotembelea kaburi la Marehemu Idrissa Ngulungu.
 Kutoka kulini ni Masatu,Huseini Ngulungu,Kassa Mussa, Ally Jangalu na beki wa zamani wa Reli Hamisi Malifedha
 Wadau wa Soka Mkoa wa Morogoro walioambatana na Wachezaji hao Wakiomba dua kwenye kaburi la Marehemu ldrissa Ngulungu
      Doglasi,Muhani
                                                 Ally Jangalu
   Kassa Mussa akiangua kilio,
 Kassa Musa akihojiwa na waandishi wa habari,ambapo alishindwa kuzungumza na waanidshi hao kwa muda mrefu baada ya kushikwa na uchungua na kuamu kuangulia kilio 
               Mohaned Mtono[kushoto] na George Masatu

Kaburi la mpwa wake ldrissa Bi.Leila ambao walikufa siku moja kwenye ajali ya gari ..MATUKIO NA MICHAPO BLOG

No comments:

Post a Comment