Search This Blog

Thursday, October 24, 2013

MANCHESTER UNITED YAIFUNGA REAL SOCIEDAD,YAMSHUKURU IÑIGO MARTÍNEZ KWA BAO LA KUJIFUNGA.Pamoja na kupata ushindi kiduchu lakini ulikuwa ushindi muhimu sana kwa kocha David Moyes kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake usiku wa jana kwenye dimba la Old Trafford,Wayne Rooney alikuwa anazunguka kila kona ya uwanja pia kiungo Mjapan Shinji Kagawa hapo jana usiku alicheza vizuri sana.


Real Sociedad pia walitengeneza nafasi za kufunga na hii ni mechi ya pili mfululizo kikosi cha Moyes kimeonyesha udhaifu mkubwa wa kumiliki mpira kwenye sehemu ya katikati kitu ambacho kimeipelekea Man Utd kushindwa kutengeneza nafasi rahisi za kufunga mabao.

Meneja wa Manchester United hivi karibuni kwenye mchezo dhidi ya Southampton alipewa shutuma  kutokana na kitendo cha kufanya mabadiliko ya kuwatoa washambuliaji na kuingiza mabeki ili kukaba,kitendo kile kilizua mijadala juu ya maisha ya baadae ya wachezaji Javier Hernández na Shinji Kagawa ndani ya klabu hiyo.Kwenye mchezo dhidi ya Sociadad wachezaji hao wote walianza huku Robin van Persie akipumzishwa ili apone kabisa majeraha yanayomsumbua,Hernández alishirikiana na Rooney kuongoza mashambulizi wakati Kagawa akichukua nafasi ya Adnan Januzaj na kucheza kiungo cha kushoto. 

Giggs kucheza na Carrick kwenye sehemu ya kiungo bado kunaonekana kutoisaidia timu.

Pamoja na ushindi wa jana bado Man utd ina kazi kubwa ya kukijenga kikosi chake ili kiweze kurudia hali iliyozoeleka.

No comments:

Post a Comment