Search This Blog

Sunday, October 20, 2013

LIVE MATCH CENTRE: YANGA 3 - 3 SIMBA FULL TIME


Dk 90+5 FULL TIME! Simba 3-3 Yanga 

Dk 83 GOOOOO.....! Gilbert Kaze anaipatia Simba bao la tatu akiunganisha krosi safi ya faulo iliyopigwa na Chollo. Simba 3-3 Yanga. 

Dk 72 Mpira umebadilika na Simba sasa wametawala mchezo. 

Dk 67 Mpira umesimama kwa muda baada ya Tambwe kuumia. 

Dk 64 Ngassa anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa. 

Dk 61 SUB: Yanga imefanya mabadiliko ametoka Kiiza ameingia Simon Msuva. 

Dk 60 YELLOW CARD...! Singano anaonyeshwa kadi ya njano. 

Dk 59 Simba wamebadilika na wanacheza soka safi sasa. 

Dk 57 GOOOOO.....! Joseph Owino anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa kichwa. Simba 2-3 Yanga. 

Dk 56 Simba inapata kona. 

Dk 54 GOOOOO....! Mombeki anaipatia Simba bao la kwanza akimalizia pasi nzuri ya Tambwe. Simba 1-3 Yanga. 

Dk 53 Niyonzima anakosa bao la wazi. 

Dk 48 SUB: Simba imefanya mabadiliko wametoka Abdulhalim Humud na Chanongo wameingia William Lucian na Said Hamisi. Simba 0-3 Yanga 

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA! 

Half time - Yanga 3 - 0 Simba 

Dk 45 GOOOOO....! Kiiza anaipatia Yanga bao la tatu akiunganisha vyema pasi ya Kavumbagu. Simba 0-3 Yanga. Simba 0-3 Yanga. 

Dk 43 Cannavaro anamchezea rafu Amisi Tambwe. 

Dk 41 Licha ya Yanga kuongoza kwa mabao 2-1, mashabiki watatu wa Yanga wamezimia na kupewa huduma ya kwanza. 

Dk 41 Chanongo anamchezea rafu Mbuyu Twite wa Yanga. 

Dk 38 Yanga wanapiga pasi 18 bila Simba kugusa. 

Dk 35 GOOOOOO.....! Kiiza anaipatia Yanga bao la pili akiunganisha mpira uliodokolewa na Kavumbagu aliyeugusa mpira uliorushwa na Mbuyu Twite. Simba 0-2 Yanga. 

Dk 32 YELLOW CARD...! Mkude wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano. 

Dk 26 David Luhende anakosa bao la wazi baada ya shuti lake kutoka nje kidogo ya lango la Simba. 

Dk 25 Kiiza anamchezea rafu Chanongo. 

Dk 24 Yanga inapata kona lakini Simba wanaokoa. 

Dk 23 Kavumbagu anakosa bao la wazi baada ya kipa Dhaira kuwahi kuudaka mpira. 

Dk 18 Kavumbagu anamchezea rafu Ramadhan Chanongo. 

Dk 15 YELLOW CARD...! Ngassa anaonyeshwa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda. 

Dk 14 GOOOOOO....! Mrisho Ngassa anaipatia Yanga bao la kwanza akiunganisha vyema krosi ya Kavumbagu. Simba 0-1 Yanga 

Dk 13 Timu zinashambuliana kwa zamu lakini kazi ipo kwa Cannavaro na Mombeki. 

Dk 9 YELLOW CARD...! Mombeki anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Cannavaro. Rafu hii ni ile ya kwanza. 

Dk 7 Betram Mombeki wa Simba anapiga kichwa langoni kwa Yanga lakini kipa Ali Mustapha anaudaka mpira. 

Dk 7 Niyonzima anamchezea rafu Abdulhalim Humud wa Simba. 

Dk 4 Ngassa anapiga krosi safi langoni kwa Simba lakini Kiiza anachelewa kuunganisha. 

Dk 3 Jonas Mkude anamchezea rafu Mrisho Ngassa wa Yanga. 

Dk 2 Yanga wamecheza pasi 10 bila Simba kugusa. 

Dk 00 MPIRA UMEANZA! 

KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA

Barthez, Twite, Luhende, Cannavaro, Yondani, Chuji, Niyonzima, Domayo, Kavumbagu, Ngassa, Kiiza 

Subs: Deogratia Munisi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Simon Msuva, Rajab Zahir, Jerson tegete, Nizar Khalifan 

KIKOSI CHA SIMBA KINACHOANZA
Dhaira, Cholo, Shamte, Kaze, Owino, Mkude, Singano, Humud, Mwombeki, Tambwe, Chanongo 

Subs: Abuu Hashim, Hassan Khatir, Issa Rashid, Zahoro Pazi, Amri Kiemba, Said Hamisi, William Lucian 

5 comments:

  1. Rekebisha hapo Kwenye Danika ya 41

    ReplyDelete
  2. Hongera Bwana Dauda kwa kutujuza... kwa kweli tunashukuru

    ReplyDelete
  3. Yaani hapo ndo naamini kuwa we Shafii ni yanga damdam, kwani ulikuwa unatujuza vizuri sana dakika hadi dakika. Lakini simba walivoanza kusawazisha yale magoli, ukaanza kuingia uvivu wa kutujurisha dakika hadi dakika. Ulivotoka dakika ya 72 mpaka dakika ya 83 - hadi full time. Lakini yote ni baada ya Simba kuanza kurudisha magoli.

    ReplyDelete
  4. ungefaa kuchukua nafasi ya malinzi

    ReplyDelete
  5. acha ushabiki wa simba na yanga ripoti mir.

    ReplyDelete