Kamati
ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana
jana (Oktoba 13 mwaka huu) kusikiliza maombi ya mapitio (revision) na mwongozo ya
uamuzi wa Kamati ya Maadili.
KIONGOZI WA
MWENGE AFUNGUA KITUO CHA IDYDCC
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Juma Ali Amir amefungua kituo cha kwanza cha
Football for Hope kilicho mkoani Iringa kwa kuwataka wananchi kukituia vizuri
ili wanufaike na huruma za kijamii zinazotolewa na taasisi ya IDYDC pamoja na
kuendeleza mpira wa miguu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kituo hicho jana (Oktoba 13 mwaka huu), kiongozi huyo
amesema taasisi ya IDYDC (Iringa Development of Youth, Disabled and Child Care)
wamefanya vizuri kuamua kutumia mpira wa miguu kusaidia jamii kwa kuelimisha
juu ya mambo mbalimbali kama ugonjwa wa ukimwi, kusaidia walemavu, haki za
watoto na afya ya jamii.Naye Mwakilishi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Patrick Onyango amesema amefurahishwa na kukamilika kwa kituo ambacho kitasaidia jamii.
Amesema idadi kubwa ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo inadhihirisha ni kiasi gani kituo hicho kitakuwa na matokeo mazuri kwa jamii.
Onyango
alisema hicho ni kituo cha 14 kukamilika kati ya 20 vinavyojengwa barani Afrika
ikiwa ni mpango wa FIFA kurudisha kwa jamii mafanikio iliyopata kwenye fainali
za kwanza za Kombe la Dunia barani Afrika.
Kituo hicho kina uwanja mdogo wa mita 20 kwa 40 uliowekwa nyasi bandia, jengo lenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya semina, chumba cha kupimia ukimwi, chumba cha ushauri nasaha, maktaba na ofisi.
Zaidi
ya dola 270,000 za Marekani zimetumika kukamilisha ujenzi wa kituo hicho
kilicho eneo la Mtwivila, Iringa mjini.
KESSY
KUSIMAMIA MECHI YA KOMBE LA DUNIA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Mtanzania Lina Kessy kuwa kamishna wa
mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20
kati ya Botswana na Afrika Kusini.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Botswana kati ya Oktoba 25
na 27 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi hiyo namba
tisa.
Waamuzi
hao wataongozwa na Pamela Majo atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi msaidizi
namba moja ni Rudo Nhananga, namba mbili ni Stellah Ruvinga na mezani atakuwepo
Tambudzi Tavengwa.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment