Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima ameanza rasmi kuziona fursa za kibiashara zilizopo hapa nchini katika sekta ya michezo.
Kwa kuanza kiungo huyo amefyatua T-SHIRT kibao ambazo zitaingia rasmi sokoni siku ya Juma pili kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga.
Meneja wa mchezaji huyo Imamu Abbas ameuambia mtandao huu kuwa bei ya T-SHIRT hizo ni shilingi za Kitanzania 20,000/=
'' Haruna Niyonzima ni mchezaji anayekubalika ndani na nje ya nchi,kuna miradi mingi tumeiandaa kwa ajili ya mashabiki wa soka hapa nchini na nje ya mipaka ya Tanzania kwa kutumia jina la Niyonzima,kwa kuanzia tutawauzia T-shit mashabiki wa soka kwa bei ya chini kabisa Tsh 20,000 ''.
Safi kaka,tumia fursa.
ReplyDeletewaswas wangu zitachakachuliwa usiku wa leo na ikifika jumapili feki zitakua nyingi sana kwa kweli watanzania lazima tubadilike tuache kutumia fursa za wenzetu vibaya
ReplyDelete