Search This Blog

Tuesday, September 3, 2013

MAKALA: ' GRACIAS' BRENDAN RODGERS...JE ATALETA KOMBE BAADA YA MIAKA 23



Na Baraka Mbolembole
Liverpool iliifunga Manchester United, na kukalia kiti cha uongozi wa ligi kuu England. Bao lilifungwa dakika ya tatu ya mchezo na mshambuliaji, Daniel Sturridge lilitosha kuwafanya, ' The reds' kupata ushindi wa asilimia 100, katika michezo mitatu ambayo tayari imechezwa na kila timu katika ligi hiyo hadi sasa.
Kazi nzuri ambayo Liverpool waliifanya kipindi cha kwanza, na wakafanya jitihada kubwa katika kuzuia kwa muda mwingi wa kipindi cha kwanza, iliwapata pointi tatu muhimu. Daniel Agger, alikuwa makini, na Martin Skrtel alikuwa bora. Walinzi hao walicheza vizuri na kumzima Robin Van Persie, huku wakimchezea ‘ kindava’ mshambuliaji huyo wa United na kupelekea akapandwa na hasira na kutoka mchezoni, hali ambayo ilifanya mechi iwe ngumu zaidi kwa United ambayo ilifanikiwa kupiga mashuti 11, lakini ni manne tu ambayo yalikuwa ‘ on target’.
Kwa upande wa United, hawakutengeza nafasi nyingi za kufunga. Luis Nani ambaye aliingia katika kipindi cha pili na kucheza mchezo wake wa kwanza msimu huu alijaribu kutengeneza nafasi za kufunga. Tatizo lilikuja ni timu kukosa namba kumi, na ni wazi kuwa kuumia kwa mlinzi Phill Jones kulivuiruga mipango yote ya kocha David Moyes ambaye hajawahi kushinda katika mchezo wa ligi kuu katika uwanja wa Anfield.
  
Namna Steven Gerrard alivyotawala uwanja dhidi ya Man United

Steven Gerrard ambaye alikuwa mchezaji bora wa mechi hiyo aliweza kuongoza kiungo cha Liverpool na alikuwa kiongozi shupavu na mwenye umakini mkubwa katikati ya uwanja, aliwaongoza viungo wenzake, Lucas Leiva, Jordan Hernderson,, na Phillipe Coutinho na kufanya safu ya kiungo ya United iliyokuwa chini ya Tom Cleverley na Michael Carrick kushindwa kusonga mbele katika muda mwingi wa kipindi cha kwanza.
Daniel Sturridge alifunga bao pekee, mwanzoni tu mwa kipindi cha kwanza na mshambuliaji huyo aliyekuwa akisaidiwa kwa mbali na Iago Aspas aliweza kuwatesa walinzi, Rio Ferdinand na Nemabnja Vidic ambao walicheza vizuri katika kipindi cha pili, lakini waliteswa na mshambuliaji huyo mwenye kasi, nguvu na ujanja wa kumiliki mpira. Sturrdge ambaye alisajiliwa mwezi, januari mwaka huu, aliweza kufunga bao lake la tatu msimu huu baada ya kuamisgha njiani mpira wa kichwa uliokuwa umepigwa na mlinzi, Agger ambaye aliunganisha kona ya Gerrard.
United walikuwa bora lakini kiwango cha chini kutoka katika safu ya kiungo iliwanyima nafasi ya kupata walau pointi moja, katika kipindi cha kwanza walionekana kuzidiwa, na kasi ya Liverpool ambao  walianza mchezo kwa kasi. Coutinho alicheza kwa ‘ mtindo wa Kibrazil hasa’ mara zote alipokuwa na mpira alisonga nao mbele, alimfanya Cleverly kutojua amkabe nani, Aspas, ambaye alikuwa katika kiwango kizuri alicheza kwa mtindo wa kuhama katikati na kukimbilia pembeni, huku Coutinho akikimbia na mipira pembeni na kuacha nafasi kwa Gerrard, kusogea katika eneo la nje ya mita 18 la United.
Ilikuwa ni Liverpool yenye kasi, mchezo wa kiingereza ulioambatana na ufundi wa kibrazil, lakini ni mapema mno kusema watatoa matunda gani msimu huu. Shukrani kwa mipango mizuri ya kocha Brendan Rodgers ambaye amekamilisha usajili wa nyota Victor Moses na Mamadou Sakho.   Simon Mignolet alikuwa imara na alitua langoni ni moja kati ya makipa bora kwa sasa katika ligi kuu England, aliweza kuokoa michomo mingi ya United na alicheza kiufundi kiki iliyokuwa imepigwa na Nani. Kipa huyo raia wa Ubelgiji aliweza kuokoa mara nne na kuinyima United walau pointi moja. Ni muendelezo wa usajili makini ambao umekuwa ukifanya na kocha, Rodgers. Jamani, muda bado, ila Liverpool inatoa taswira nzuri.
   


. Liverpool,  walitumia ufundi na nidhamu ya mchezo hasa katika eneo la kiungo ambalo Gerrard, alionekana kwenda sambamba na kina Michael Carrick na Tom Cleverley, hata katika eneo lao la ulinzi, walionekana kucheza kwa nidhamu kubwa huku Coutinho akichezesha timu pamoja na Jordan. Kwa, United kama kawaida yao hupendelea kumaliza mechi mapema, lakini wakakutana na umakini wa safu ya kiungo na ulinzi ya Liverpool ambao walikuwa imara kama wanacheza mechi ya fainali, kumbe ni mechi ya tatu tu kati ya 38 za msimu. United, kama kawaida yao njia yao kuu ya kujilinda ni kufanya mashambulizi ya haraka, na bila shaka Rodgers alitambua David Moyes angeendeleza falsafa alizozikuta klabuni hapo na kuichezesha United kwa mtindo ule ule wa Alex Ferguson.
ROONEY? Wayne, amebaki baada ya kelele nyingi kuwa angeondoka, na katika mchezo dhidi ya Liverpool United walionekana ‘ kum’ miss’, inawezekana Shinji Kagawa asipate nafasi kubwa ya kucheza msimu huu, lakini chaguo bora la pili katika namba kumi baada ya Wayne ni Mjapan huyu,  United inamuhitaji zaidi Wayne.
Miaka 23 sasa imepita tangu Liverpool walipopata ubingwa wao wa mwisho wa ligi kuu, si rahisi kutwaa taji msimu huu, lakini kwa nini nisiseme’ Shukrani, Brendan Rodgers? Liverpool, Arsenal, Manchester City, United, Chelsea, Tottenham, zote ni timu kali msimu huu.
 0714 08 43 08

No comments:

Post a Comment