Search This Blog

Sunday, August 4, 2013

SAKATA LA AZAM TV VS YANGA: VILABU VYOTE VYA LIGI KUU VYAIPINGA YANGA - WAUNGA MKONO AZAM TV KUONYESHA LIGI - HIZI NDIO SABABU ZAO


KATIKA siku za karibuni, kumekuwapo na mjadala kuhusiana na hatua ya klabu ya Yanga kupinga udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania unaotarajiwa kufanywa na Azam Media.

Tumeona ni vema tukatoa msimamo wetu wa pamoja kuhusiana na hatua hiyo ya wenzetu kwa lengo la kuweka rekodi sawa.

Tunataraji hatua hii ya vilabu hivi 13 itafunga mjadala huu na tungependa wana habari, kama mtaamua kuuendeleza, basi muundeleze katika mrengo ambao wadau, yaani sisi vilabu vinavyoshiriki mashindano hayo, zimeamua kuufuata.

Tunapenda kukumbusha kwamba kwa muda mrefu, kilio cha vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania vilikuwa ni ukosefu wa wadhamini na kwa bahati nzuri kuna dalili kwamba Mungu ameanza kukisikia kilio hicho msimu huu.

Kwa faida ya umma, tungependa kutoa takwimu za nchi jirani zinazotuzunguka. Kenya, kila klabu hupata Sh milioni saba za Kenya (sawa na Sh milioni 125 za Kitanzania) kwa mwaka –fedha ambazo zimeifanya ligi ya Kenya kuwa na uwiano na ushindani wa kweli (fedha hizo ni mjumuisho wa gharama za matangazo ya televisheni na udhamini wa bia ya Tusker).

Tanzania leo tunajivunia kuwazidi Kenya kutokana na udhamini wa Azam ambapo kwa mwaka huu, kila klabu itapata zaidi ya Sh milioni 170 (Jumla kutoka milioni 100 za Azam na milioni 70 za Vodacom).

Hatuna sababu ya kutaja viwango vya udhamini kwa nchi nyingine jirani kama Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia nk kwa vile zote zina udhamini wa chini kuliko Kenya.

SuperSport, ambao wanaliliwa na baadhi yetu, udhamini wao kwa ligi ya Uganda ni dola 350,000 ambazo ni pungufu kulinganisha na dola milioni moja zilizotolewa na Azam Media hapa nchini.

Ni imani yetu kwamba udhamini huu utaifanya ligi ya Tanzania kuwa bora kuliko zote za Afrika Mashariki. Hili litasaidia kutengeneza timu bora ya Taifa ya Tanzania.

Tungependa kutoa ufafanuzi wa masuala machache ambayo yaliongelewa na wenzetu wa Yanga kama sababu za kupinga udhamini huu.

BODI YA TPL

Kwa mujibu wa Katiba za FIFA, CAF na TFF, Haki za Televisheni zipo chini ya FA ya nchi husika. TFF iliamua kukasimu shughuli ya majadiliano kwa Kamati ya Ligi ambayo ilishirikisha vilabu vyote 14, ikiwamo Yanga na wawakilishi wake walihudhuria mchakato mzima hadi mwisho.

Hoja ya Yanga kuwa bodi haina nguvu/Mamlaka kisheria kwa kuwa ni ya mpito inakosa mashiko kwa sababu kimsingi ni TFF ndiyo iliyoingia mkataba kwa sababu ndiyo iliyopewa mrejesho na Kamati ya Ligi kwamba mchakato umekwenda sawasawa.

Hoya ya kuwa Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA. Hili si kweli hata kidogo. Mmoja wa wajumbe wa TPL ni Seif Ahmed almaarufu Seif Magari; ambaye vyeo vyake ndani ya Yanga vinajulikana.

Kama alikuwa hahudhurii vikao vya TPL, hilo ni suala la Wanayanga wenyewe kumuhoji kwanini alikuwa hahudhurii hivyo na hivyo kuinyima klabu yake ushiriki katika mijadala muhimu kwa maslahi ya soka hapa nchini.

Ifahamike pia kwamba TPL haikuhodhi mchakato huu bali ilitoa fursa kwa vilabu vyote vya Ligi Kuu kushiriki ambapo Yanga ilikuwa ikiwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wake, Clement Sanga na Katibu Mkuu, Lawrance Mwalusako.

Hii maana yake ni kwamba hoja kuwa Yanga haikushirikishwa ni mfu.

Yanga walitumia neno UTARATIBU WA DUNIA NZIMA wakisema eti hakuna mahala duniani ambapo kampuni yenye klabu inayocheza ligi husika kupewa mkataba wa udhamini au urushwaji wa matangazo. 

Inaonekana Yanga hawakufanya utafiti kwani ligi ya Afrika ya kusini ina timu inayoitwa Super Sports United na inarushwa na kituo cha TV chaSupersports.

Pia majirani zetu Kenya wana timu inayoitwa Tusker FC huku ligi hiyo ikidhaminiwa na bia ya Tusker. 

Tunawashauri Yanga kuwa ni vema kufanya utafiti kabla ya kuibuka na hoja za namna hii ili kuepuka kuwapotosha wanachama wao.

Yanga pia katika hoja zao wamepinga utaratibu wa kugawana mapato sawa. Hoja hii ni ya msingi na majadiliano yetu yalilitazama hili kwa kina lakini tukaona kwa mazingira ya Tanzania na uchanga wa ligi yenyewe kwa sasa ni heri kugawana sawa ili pesa kwa usawa ili itoke kwa wakati na kusaidia vilabu kujiendesha. Yanga wanakosea wanaposema eti wao wanastahili kupewa zaidi kwa sababu ni klabu kubwa na yenye mashabiki wengi kwa kuwa sababu hii haitumiki sehemu yoyote duniani.

Tuchukulie mfano wa nchi ya England ambako ingawa Liverpool ina washabiki wengi kuliko Manchester City na Chelsea, imezidiwa kwenye mapato ya televisheni na timu hizo.

Hii ni sababu kinachoamu mapato mwisho wa siku ni kiasi cha mechi za timu ambazo zimeonyeshwa na televisheni kwenye msimu husika na nafasi ya timu kwenye msimamo wa ligi. 

Hata hivyo, ikumbukwe kwamba nchini England, malipo haya hufanyika baada ya msimu kumalizika na hapo ndipo watu hukaa chini na kupigiana hesabu za nini kilipatikana. Sasa ukitumia mfumo huu, ina maada timu zitalazimika kusubiri ligi iishe ili kuangalia msimamo ya ligi kisha kugawana mapato. Sote tunajua jinsi timu zinavyoteseka kwa kukosa nauli, posho, mishahara, pesa za kambi nk.

Kwa mazingira yetu ya Tanzania kwa sasa, mfumo kama huu haufai. Hii ni kwa sababu timu zinahitaji fedha kuanzia kwenye maandalizi ya mechi ya kwanza na hazikopesheki fedha kwenye mabenki.

Tanzania inachohitaji kwa sasa ni ligi yenye ushindani tofauti na sasa ambapo ushindani uko kwa timu chache zenye uwezo wa kifedha.

Tukizijengea uwezo timu zote taifa litakuwa na ligi nzuri na hatimaye timu nzuri ya taifa. Pia itawezesha wadhamini wengi zaidi kuingia kwenye mpira na hivyo timu nyingi zaidi kufaidika.

Tukifikia huko, tunaweza kukaa chini na kutazama mfumo wa kugawana mapato utakaokuwa bora zaidi wakati huo.

Mambo ya Kuzingatia.Tangu ligi ianze hapa nchini takribani miaka 50 iliyopita, hakuna timu iliyowahi kulalamikia mfumo wa kugawana mapato sawa kwa kila mechi ambao umekuwa ukitumika. Mfano mapato ya mlangoni tumekuwa tukigawana sawa na Yanga haijawahi kulalamika, Pesa za udhamini wa Vodacom tangia ilipokuwa ikidhaminiwa na TBL hadi leo hii tumekuwa tukigawana sawa na Yanga haijawahi kulalamika kutaka kupata zaidi kwa kuwa eti ina mashabiki wengi, pia hata pesa za haki ya matangazo ya Televisheni zilizowahi kutolewa huko nyuma nailiyokuwa ikiitwa GTV, na Star TV kwa nyakati tofauti pesa ziligawiwa sawa kwa kila timu.

Hii ni kwa sababu kikanuni, timu zote zinazoshiriki kwenye ligi ni sawa na zote zinaweza kuwa bingwa au kushuka daraja. 

Ni mdudu gani huyu aliyeingia kwenye soka ya Tanzania na kuanza kuleta siasa za kubaguana? Baba wa Taifa alipata kutuasa kwamba dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu. Ikianza, haitaishia kwenye ligi pekee na itakwenda hadi mahali tusipotaka.

MGOGORO WA MASLAHI

Yanga imekuwa ikilalamikia uwepo wa kiongozi mwandamizi wa makampuni ya Bakhresa kwenye bodi ya Ligi na kusema inaleta mgongano wa maslahi.

Sisi vilabu tunaamini kwamba uwepo wa kiongozi huyu ndiyo umesaidia makampuni yake kuwekeza fedha kwenye mpira. Na mifano ipo hai tukianzia na michuano ya Vijana ya Uhai Cup, ujenzi wa kituo cha michezo cha Chamazi ambacho kinatumiwa na timu nyingi za Tanzania. 

Na sasa tunafaidika na udhamini huu mnono ambao haujapata kutokea katika historia ya Tanzania.

Tungependa viongozi wengi zaidi wa makampuni yanayoheshimika hapa nchini wakijitokeza kuongoza mpira badala ya kuanza kuwapinga.

Kwa mfano, tungependa kuona mkurugenzi wa benki ya CRDB akiwa kiongozi wa Ashanti, bosi wa Barrick akiongoza Mbeya City na Mkurugenzi wa Tanga Cement akiongoza Coastal Union.

Hivi ndivyo namna mpira unavyoweza kuvutia wawekezaji. Ndiyo maana tulifurahi wakati Yusuf Manji, alipoomba uongozi Yanga.

Bado tunataraji kwamba naye atajitosa kuingiza fedha zake kwenye ligi ya Tanzania (mpira) kama alivyofanya Bakhresa ambaye pamoja na kutumia fedha zake Azam FC, bado ameamua kusaidia na timu nyingine kwa ujumla.

Tunapenda kumuahidi Yusuf Manji kwamba iwapo naye atataka kudhamini Ligi Kuu iwe kibiashara au kiufadhili, sisi tutamuunga mkono na hatutajali suala la mgongano wa maslahi.

UPOTEVU WA MAPATO

Wenzetu Yanga wamedai kwamba kwa kuonyesha mechi kwenye televisheni, mapato yake ya mlangoni yatapungua.

Hili pia halikufanyiwa utafiti wa kutosha. Katika siku za karibuni, mechi zilizoingiza mapato makubwa zaidi ya milangoni ni zile ambazo zilionyeshwa Live kwenye televisheni za ndani na nje ya nchi.

Mifano ni mechi za watani wa jadi msimu uliopita zilizoonyeshwa Live na SuperSport na mechi za Kombe la Kagame zilizoonyeshwa wakati huo.

Hata mechi ya Taifa Stars na Ivory Coast iliyoonyeshwa Live pia, ilijaza uwanja. Ulaya ambako karibu kila familia inamiliki televisheni na umeme wa uhakika, bado watu wanajaa katika viwanja vya soka.

Mpira kuonyeshwa kwenye televisheni unaufanya utangazike zaidi na watu watake kuona. Kuna faida nyingi za mpira kuonyeshwa kwenye televisheni kuliko hasara moja ya kufikirika ambayo Yanga wanaiona.

Ingekuwa vema iwapo Yanga wangetoa takwimu za kuonyesha ni kwa namna gani mechi kuonyeshwa kwenye televisheni kuliwahi kupunguza mapato ya milangoni.

Kwa faida ya umma, mpira kuwa kwenye televisheni kuna faida zifuatazo; jezi kuongezeka thamani na hivyo kuvutia makampuni makubwa kutaka kudhamini klabu wakitumia fursa ya kutangaza bidhaa zao, matangazo ya viwanjani (touchline fence) kuwa na thamani zaidi ambapo kwa sasa vilabu havipati chochote, kuchochea michezo ya kubahatisha, kutabiri matokeo na kupata habari kupitia simu za mkononi na hivyo vilabu vitaanza kutengeneza fedha za kutosha.

Ulaya wamesonga mbele kutokana na televisheni. Anayekataa mpira kuonyeshwa kwenye televisheni ni sawa na mtu anayegoma kutumia mfumo wa digitali katika ulimwengu wa leo. 

UWAZI KWENYE MCHAKATO WA KUUZWA KWA HAKI ZA MATANGAZO
Yanga wameandika kwenye taarifa yao rasmi eti hakukuwa na uwazi kwenye mchakato wa kuipata kampuni ya kurusha matangazo ya Televisheni.

Sote tunajua kuwa vituo vya televisheni vilivyopo nchini kama Star TV ambayo iliwahi kurusha mechi kadhaa msimu uliopita vilikuwa vikijua kuwa kuna nafasi hiyo na TFF mara kadhaa wamekuwa wakitangaza hilo kupitia idara ya Habari ya TFF.

TFF kwa mfano walikwenda mbali kwa kuialika Supersports kuja kuonesha mechi bure kwa kilichokuwa kikiitwa Super Week ili kuwashawishi waje kuwekeza na mara ya mwisho ni Yanga hawa hawa walioongoza harakati za kuikataa Supersports kuonesha mechi bure wakisema kuwa kama ni kuwavutia inatosha. 

Katika mazingira kama haya tunastaajabishwa na ukigeugeu wa Yanga leo kusema eti tenda haikuwekwa wazi. Sote tunajua kuwa ni Super Sports pekee tuliokuwa tukiwategemea na kuwashawishi ambao hawakuonesha kuhitaji kuja kuwekeza. Kwa nini leo tuikatae Azam TV?

Yanga wanaposema eti TFF/Kamati ya Ligi imeipa haki za matangazo kampuni ambayo haina ofisi wala kituo cha televisheni kilicho hewani kwa sasa wanasahau kuwa huko nyuma TFF iliwahi kuwapa haki za matangazo GTV ambao hawakuwa na ofisi wala kitu cha TV na baada ya miezi michache walifungua ofisi zao na kuleta vingamuzi na kuaza kurusha mechi zetu. Vilabu vilifaidi udhamini ule kabla ya ile kampuni kufilisika. Kwa hiyo hii si mara ya kwanza kwa jambo hili kufanyika na kama Azam TV hawataonesha mechi za ligi hiyo sisi kama vilabu haituhusu kwani ni hasara yao.

Tunachowaomba Azam Media sisi kama vilabu ni kuhakikisha wanatulipa pesa zetu kwa haraka ili zitusaidie kwenye maandalizi,Tunawaomba Yanga wasichafue hali ya hewa kwa kuwa wao hawana shida ya Pesa.


Sisi Umoja wa Vilabu 13 vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania tunapinga, kwa nguvu zote, madai ya Yanga kwamba hatukushirikishwa kama vilabu kwenye mchakato huu.

Mfumo wa ugawanyaji wa mapato tuliouchagua, tuliuchagua wenyewe bila kushurutishwa na yeyote na tunadhani ndiyo mfumo unaotufaa kwa sasa hadi hapo ligi yetu itakapokuwa na nguvu maana kwa sasa inaruhusiwa klabu kupata fedha mwanzoni kulingana na hali halisi ya vilabu vyetu.

Tunawashauri wenzetu wa Yanga waanze kuamini kwenye kitu kinachoitwa Uwajibikaji wa Pamoja (Collective Responsibility). Mambo yanayoamuliwa kwenye vikao hayapaswi kupingwa nje ya vikao.
Kama hoja ililetwa kwenye vikao na ikazidiwa nguvu na hoja nyingine, hakuna sababu ya kuikataa kwa sababu tu hukubaliani nayo. Mfumo wa kidemokrasia una kanuni moja kuu; Wengi Wape 

Imetolewa na

Vilabu 13 vya Ligi Kuu ya Tanzania

Simba SC, Azam FC, Ashanti United, JKT Ruvu, Ruvu Shooting Stars, Mgambo JKT, JKT Oljoro, Rhino Rangers, Mbeya City, Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar, Coastal Union na Kagera Sugar.

MWISHO

27 comments:

  1. Ni aibu kwa viongozi wa Yanga kutokuona ukweli wote huu wakawa wanaburuzwa na Manji!! Halafu mashabiki wa Yanga ndio kabisaa mbulula!! Comments zao hapo chini ndo utachoka.Ngoja waje ushuhudie...!

    ReplyDelete
  2. Yanga hawana lolote la maana kama wana hela wakae kimya!udhamini huu ni kwa mazingira ya Tanzania ni ulaya,wacha timu kama Ashanti zijikwamue na taabu

    ReplyDelete
  3. yanga wachawi tu wa maendeleo ya soka la tanzania sawa na ccm tu wachawi wa maendeleo ya tanzania kwani wamehodhi viwanja vyote vya mpira wakati hawavifanyii matengenezo.

    ReplyDelete
  4. Safi sana,nimeipenda. Yanga mechi zao zitaonyeshwa na Manji TV

    ReplyDelete
  5. safi kabisa hao yanga kama hawataki huo udhamini wajitoe kwenye ligi

    ReplyDelete
  6. Lets wait and see

    ReplyDelete
  7. Duuuuuuuuuh! kweli Tanzania noma, yaani leo tu mmeunda umoja wa vilabu 13! Unaitwaje huo umoja wenu? WENGI WAPE AMA KANUNI YA DEMOKRASIA? Ha ha ah ah ah ah a ha! Magumashi orijino, mwisho wa cku mikataba ya RICHMOND itazidi kujirudia kila kukicha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kusoma hujui hata picha huoni. Acha umbulula, UMOJA ni wa klabu zote zinazoshiriki ligi kuu, Yanga ikiwemo. Kama hawakutaka kushiriki majadiliano ili waendeleze ushamba wao ni juu yao. Wasilete umburula

      Delete
    2. Umoja wa klabu unahusisha zote 14 za ligi kuu. Kama Yanga wanapinga maendeleo na kuamua kujiweka pembeni bila sababu zinazoeleweka, waliobaki wajiite vipi?? Ni haki tu wajiite 13 kwa maendeleo yao.
      kama Yanga wao wana pesa za manji waelewe wenzao wanategemea udhamini (na ndo maana ya wengi wape), usitegemee watakataa. Na maana ya demokrasia ni kwamba Yanga walipewa nafasi ya kushiriki kwenye mahadiliano, ila kuamua mambo ni lazima kufanyike kwa utaratibu huo wa kidemokrasia. Sidhani kama Yanga walikuja na proposal nzuri zaidi hivo vilabu vingine vikagoma, sidhani. Considering the financial status of most of the 14 clubs participating in the premier league, Instead of complaining like babies, Yanga should have suggested a better proposal than that of Azam. its an offer that the other clubs can not reject at the moment, lets be honest

      Delete
    3. huo huo umoja wao ndo husubiri mapato ya mechi za yanga ili maisha yao angalau yawe nafuu.mbona mkicheza wenyewe kwa wenyewe[mburula kwa mburula]mnaishia kugawana elfu hamsini kwa hamsini,kama mapato ya mlangoni? wakati mkicheza na yanga ndo siku ambayo kwenu huwa ya neema,na sio nyie tu hata hao kamati ya ligi na kaka zao TFF.sasa hapo ukubwa wa yanga unahitajili elimu gani mtu kuujua?leo wingi wa mashabiki wake nani mwenye mashaka nao.nukuu yangu....MASIKINI HANA MSIMAMO MTAYUMBA TUU.

      Delete
    4. Ni kweli hizi klabu ni masikini. Na kwa umaskini wao ndio Yanga ambayo ina hela za kurithi za manji na za kina bin kleb, za kina riz inataka kuziendesha. Wakiacha huo mkataba watapata wapi milioni 100 nyingine?? Yanga watoe pendekezo wapi zitapatikana hela zaidi ya hizo na sio kuleta hoja za kitoto. Hoja hazina kichwa wala miguu. Watu wanalia njaa kila siku, leo wanapata deal mnaleta hoja za kijinga, au wanataka waendelee kuwa masikini ili wawafunge kirahisi??!!

      Delete
  8. Yanga wamebugi, hawana sababu za msingi, ni ushamba tu na vurugu zisizo na maana

    ReplyDelete
  9. ADANTE...ILA MBONA HAWAJAJIBU HOJA KUWA AZAM TV INAANZA LINI NA ITAKUWA CHANNEL GANI...?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii hoja haina mashiko, Yanga tu wanajaza sababu kibao ili waonekane wana pointi. Kwani ukipewa hela na TV ukatia kibindoni halafu mechi yako isionyeshwe nani anapata hasara, klabu au TV?? Muwe mnafikiri hata kidogo

      Delete
  10. Afadhali wamegundua janja ya Yanga!! Wenyewe yanga wana udhamini mpaka wa chama chetu,plus Manji so wasijaribu kuwashka wenzao maskio wakt wao mpunga upo wa kutosha!

    ReplyDelete
  11. 1.Mimi kama mpenda maendeleo ya michezo kwa suala la yanga kutaka kugoma kuonyeshwa kwa ligi na Azam TV nadhani wanataka kutunyima haki wapenzi wa mpira tulioko mikoani na sababu wanazotoa hata hazieleweki. Hivi hawa viongozi wa yanga ni viongozi wa mpira au siasa maana haiwezekani kwa suala lenye kuleta neema au mapinduzi ya soka eti wao wanaandika barua mpaka kwa rais hivi wana uelewa wa mpira hawa watu kweli
    2 kama yanga wataendelea na msimamo wao nadhani mechi ambazo watakuwa wenyeji ndio zisionyeshwe ndio wenye haki nazo ila za ugenini zionyeshwe.

    ReplyDelete
  12. Mdogo Wangu Shaffy, Vilabu vimepokea hilo Deal Kama Zawadi Vile. Na sio majadiliano ya KIBIASHARA. HAVIJITAMBUI NA HAVIONI THAMANI YA PRODUCT YAO AMBAYO NI LIGI.

    NAWAHURUMIA YANGA, HAKUNA UMOJA HAPO. AZAMA NDIO AZAM NDIO MKOMBOZI WA LIGI YETU. TUSUBIRI MWISHO WAKE WATAGUNDUA MAKOSA YAO

    ReplyDelete
  13. kabla ya hoja ya Galileo watu waliamini kuwa jua linazunguka dunia, na yaliyomkuta wengi tumeyasoma lakini mwisho wa siku wote leo tuna kubali kuwa dunia inazunguka jua..kuwa na hoja ambayo ipo tofauti na wenzako haimaanishi siku zote kuwa unakosea..tunaweza kusema wengi wape lakini haimaanishi kuwa siku zote wako sahihi...na siku zote mtu uunga mkono au ukubali kile kinachofanana na anacho kiamini...deal ya Azam TV mtu anaweza kuiunga mkono pale tu anapoona inaenda kujibu anayoyafikilia..mfano nasoma watu wengi wanasema eti deal ya Azam TV ndo mkombozi wa soka la bongo...inawezekana ikawa ivo na ueanda isiwe ivo...pointi inayoletwa na Yanga lisaidie kufikiria zaidi ...milioni 100 (kama niko sahihi) si nyingi kivile...ila inaweza kuwa nyingi kwa mazingira ninayo yaona....vilabu vingi ni masikini sawa lakini mpango wa kuvisaidia usiviumize vilabu vingine..lakini hapa ikumbukwe kuwa hili deal la Azam ni biashara...siri ya ni vp Azam TV itanuafaika na deal hili ..hakuna nayejua zaidi ya Azam TV tu...hauwezi kutoa 100 milioni kwa kila kilabu ya ligi kuu kama hakuna faida inayopatikana... kwa mtazamo wangu ni rahisi kwa Azam TV kutumia unyonge wa vilabu vilivyo vingi ili inufaike na wapenzi wa Yanga lakini bila kuilipa Yanga kile inachostahili...kama ni kusaidia vilabu ijulikane kwamba huu ni msaada na si biashara..kama ni msaada klabu ina weza kuupokea au kuachana nao..lakini kama ni biashara hicho ni kitu kingine kabisa.

    wanasema ligi ni zao (product) ya TFF kwa hiyo vilabu havina nafasi ya kuhoji au maana yake ni nini...ina maana TFF iachiwe iingie mikataba inayo hatarisha maslahi ya vilabu husika..wengi mtakuwa mnaikumbuka ishu ya yule mchezaji wa Kenya alivotaka halipwe kwasababu taswira yake ilikuwa inatumiwa kibiashara na wadhamini wa Harambe Stars, wengi walisema ni mbinafsi lakini mwisho wa siku walikubali kuwa hana haki katika alilokuwa anadai...mimi ninaona kuna haja ya kuwa makini na majibu ya jumla jumla kama tunataka kuendelea..ebu niambieni ule mkataba wa ligi ya vilabu vinane ambayo ilipaswa kuwa inachezwa kama pre-season ambayo mwaka jana Yanga ilikataa kuicheza imeishia wapi...... bado kuna tatizo sana katika mamnbo haya na hasa pale TFF....mambo yanayofanywa na TFF siyo ya kuyaamini kuna maroroso kibao..kwanza TFF hawako makini kivile kama watu wanavyodhani...we fikiria kama ishu ya uchaguzi na kurekebisha katiba yao wanaleta ubabaishaji...na ubabaishaji wao huko si kwa hili la uchaguzi na urekebishaji wa katiba ila kwenye mambo mengi...sina hakika sana kama kaika deal la Azam TV walikuwa makini...mtu atasema ni kamati ya ligi lakini mi nasema ni TFF...hata kamati ya ligi ilianza kwa mizengwe...ilitakiwa Bodi ya Ligi ili isimamie haya ...TFF wakapendekeza ianze kamati kuelekea kwenye hiyo Bodi...leo tuko wapi...na kuweka wazi mi binafsi sioni kama deal la Aam TV kuwa mkombozi wa soka la bongo kwa sababu limekaa kiunyonyaji sana kwa klab kubwa zenye mashabiki wengi ambao ndo target ya AZAM TV ili iweze kutengeneza hela ila haitaki kuwalipa kile wanachostahili.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeongea kwa kirefu sana lakini bado hujaeleza ni kwa jinsi gani hoja za Yanga ni sahihi. Hapo juu umoja wa klabu umeonyesha jinsi hoja za Yanga si sahihi. Lakini kubwa hapa ni kuwa, ita huo mkataba unavyotaka, ni biashara au msaada, kama unasaidia klabu husika wacha wakubaliane nao. Mi bado sijaona hasara ambayo hizo klabu moja moja au kwa ujumla wake wataipata iwapo watakubaliana. Yanga pia waonyeshe watapata hasara gani

      Delete
  14. Yanga wanataka kuanzisha Tv yao.

    ReplyDelete
  15. Kwenye hii deal Yanga wanataka tu kujifanya wanajua na wana nguvu kuliko mtu mwingine yoyote lakini ukweli wanachemka.
    1. Umoja huu ambao Yanga ni mwanachama umeshaamua jambo kwa pamoja Yanga lazima ile kwao, labda wangejitoa kwenye umoja kabla ya maamuzi.
    2. Timu za ligi kuu karibu zote ukiondoa Yanga Simba Azam na Mtibwa, kidogo na Kagera, zimeshateseka sana na udhamini wa fedha kiduchu zinazotolewa na wadhamini wa sasa na waliopita. hakukuwa na dalili ya fedha kuwa kubwa kukidhi mahitaji. Pamoja na kuwashukuru vodacom, hawawezi kuacha deal kama hii, tena ikiwa ndo mwanzo tu.
    3. Klabu zikiongezewa uwezo wa kifedha zitaanza kuleta ushindani kwenye ligi. Matokeo yake ni ligi kuwa bora zaidi, timu ya taifa kuwa bora zaidi, na pengine wachezaji wetu kuanza kuonekana hata na timu za nje.
    4.Yanga badala ya kuongea sababu zisizo na msingi, wapendekeze au waonyeshe mbadala wa deal kama hii ambayo vilabu vitapata pesa zaidi kuliko hii wanayotoa Azam.
    5. Mpira ni biashara, na sote tunajua biashara ni matangazo. Vodacom wanaweka matangazo yao kwenye jerzy, Azam wataweka kwenye TV yao wakati wa vipingi vinarushwa. Nina uhakika hata vodacom watafurahia deal kwa sababu watapata kurushwa bure kabisa kwani jerzy zenye nembo yao zitakuwa zinaonekana kila mahali. Je, timu za ligi kuu hazitaki kuonekana na kupata mashabiki zaidi?? hazitaki wachezaji wake wajulikane na mashabiki, na mawakala?? La hasha. Deal hii inalipa hasa ukizingatia ndio mwanzo tu. Leo tunawatambua kina ronaldo hata jinsi wanavyokimbia tu sio lazima umuone sura. Yote ni kwa sababu tunawaona kwenye TV kila kukicha.
    YANGA ACHENI UZAMANI NA USHAMBA

    ReplyDelete
  16. nashangaa kuona leo vilabu vinaungana na kutoa kauli moja.kwngu huu ni unafiki mkubwa wa viongozi wa vilabu vyetu kama kweli wana nia ya kweli ya kujikomboa kwann walishindwa kuonyesha hyo dhamira kwenye sakata la African Lyon ambao waliamua kujikomboa kutoka kwenye mkataba dhalimu wa vodacom...hapa naanza kuona mbali na watu kupigania maslahi ya vilabu kuna kitu kingine ambacho nakiona hapa maslahi binafsi kwa hawa viongozi wa vilabu vyetu na kamati ya ligi...muhimu ni kwa viongozi hawa wa TPL,TFF na YANGA kulijadili hili kwa mapana na uwazi zaidi....

    ReplyDelete
    Replies
    1. usichanganye ishu kabisa. Ishu ya African Lyon ilikuwa ishu tofauti kabisa na hii. Huu ni udhamini ambao haukinzani na mwingine wowote. Kwa mfano tu, kwa sasa si rahisi au niseme haiwezekani TV nyingine ikaingia mkataba na umoja huu kuonyesha ligi hapa tanzania, labda waonyeshe nje. Ni haki ya kimkataba ya azam tv kuweka kipengele kama hiki, ingawa si lazima wakiweke kama wakiamua. kwa lugha nyingine, hapa ikija kampuni ya magari ikataka kuingia mkataba na hizi timu, itaweza bila matatizo yoyote ya kimgongano wa kimaslahi kwa sababu biasahara yao na ya azam tv na ya vodacom, ziko tofauti sana. Hebu soma maelezo ya hiyo habari kwanza kabla hujakurupuka kusema Yanga hawakushirikishwa.

      Delete
  17. Kezzo au wapi. kezzooooo. wape vijembe haea jamaaa. wanabwabwaja sana. tafafhari kezooo

    ReplyDelete
  18. naunga mkono yanga iachane na hiyo tv ya kitapeli
    lini ilifanyiwa majaribio tukaona ufanisi wake tunachokiona mkataba umeanza .bila kuona uzoefu,tutapinga wanotaka mechi za timu ya zionyeshwe endeleni hapa sio uganda au kenya

    ReplyDelete
    Replies
    1. wakipewa hela halafu tv ikashindwa kuonyesha mechi inakula kwa nani?? Kwa Yanga??

      Delete
  19. Kezzo toa hoja. au saumu kali

    ReplyDelete