Search This Blog

Thursday, August 15, 2013

JOSE MOURINHO VS CRISTIANO RONALDO: NAMNA MAHUSIANO YALIVYOHARIBIKA WAKIWA MADRID


Ilikuwa taswira ya kusisimua sana. Cristiano Ronaldo anakimbia kuelekea kwenye benchi la ufundi la Madrid, anatanua mikono yake na anaenda kumkumbatia Jose Mournho. Mwanga wa Cameras ulitawala na mashabiki walishangilia baada ya kuona kitendo hicho cha staa wa timu hiyo kukumbatiana na kocha wake katika kuonyesha mshikamano na upendo uliopo baina yao. Lakini je tukio hili lilikuwa lina ukweli ndani yake?

Cristiano alifunga mabao yote matatu wakati Madrid ilipoifunga  Levante 3-1 mnamo February mwaka 2012 na nahodha huyo wa Ureno aliahidi kushangilia na kocha wa viungo Rui Faria ikiwa angeweza kufunga hat-trick. Hivyo wakati alipofunga goli la tatu, akataka kutimiza ahadi yake na akakimbia kwa takribani 50 yards kuelekea bechi la ufundi la Madrid, wakati Faria alipoinuka kutoka kwenye siti yake akimsubiri. Lakini Mourinho akamuwahi na kukaa mbele yake, kwa kushindwa kumfikia aliyempanga, mshambuliaji huyo ikabidi amkumbatia Special One.
 

Hapa wakizozana mazoezini


Picha ya tukio hilo lilionyesha taswira ya chanya. Lakini ukweli nyuma ya pazia, wareno hawa hawakuwa na mahusiano mazuri, huku Mourinho akisema mchezaji huyo anajiamini sana na hafurahishwi na tabia yake ya kupinga maelekezo yake ya uwanjani.


Kugombana baina ya wawili hawa kilikuwa kitu cha kawaida kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, hata katika msimu wa kwanza wa Mourinho ndani ya Bernabeu. Siku chache baada ya kushinda Copa del Rey shukrani kwa goli la Ronaldo katika dimba la Mestalla dhidi ya Barcelona, lakini wiki kadhaa nyuma ilikuwa imefungwa 2-0 na FC Barcelona katika dimba la Santiago Bernabeu. Akiwa amechukizwa na kufungwa kwa timu yake, Cristiano aliwahimiza wachezaji wenzie waachane na mbinu chafu za Mourinho na kucheza mchezo wa kushambulia zaidi. Baada ya mchezo, Mourinho alimsema sana Ronaldo kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Ronaldo alifunguka kwa waandishi wa habari baada ya mchezo kwamba hakuwa anapenda aina ya mchezo Mourinho anaowafundisha. Matokeo yake? Aliachwa kwenye mchezo uliofuatia ambapo Madrid walifungwa 3-2 nyumbani dhidi ya Zaragoza.

Kutokea hapo Mourinho alikuwa anatumia zaidi wasaidizi wake kumpa maelekezo Ronaldo, lakini baadae ikabidi wasuluhishwe na wakala wao Jorge Mendes - rafiki yao na patna wao katika biashara. Akiona mteja wake akipigwa benchi wakati akiwa katika mbio za kuwania tuzo ya Pichichi kwenye La Liga, Mendes ikabidi aingilie kati ugomvi huo.

Ugomvi ukapotea . Wote wawili Mourinho na Ronaldo walikuwa wakitengeneza fedha nyingi na kampuni ya Mendes Gestifute na ukiachana na masuala yao ya timu ya Real Madrid - kulikuwa na biashara iliyotakiwa kukua. "Hawakuwa na mahusiano ya karibu sana, waliongea mara chache sana katika kipindi cha miaka mitatu ya Mourinho ndani ya Madrid, ni Mendes aliyepooza ugomvi wao." Mtu mmoja wa karibu na Madrid alisema.

Na Mendes angeendelea kuingilia kati kwa mara nyingine. Mwezi  January mwaka huu, Mourinho alikuwa kwenye kitimoto baada ya kuanza kumeweka benchi Iker Casillas kitu kilichoplekea mgawanyiko mkubwa ndani ya Madrid. Alikosa sapoti, vyombo vya habari vya Spain pia mashabiki wote walimgeuka, hivyo alihitaji kusaidiwa. Na nani hasa angeweza kumpa msaada huo zaidi ya nyota mkubwa wa klabu hiyo? Hivyo Ronaldo akaamua kutoa goli lake kwa Mourinho katika ushindi wa
4-3 dhidi ya Real Sociedad (kwa ombi la Mendes), lakini pia aliongea hadharani kumtetea bosi wake. Wakala Mendes alimuomba Cristiano kuviambia vyombo vya habari kwamba Mourinho alikuwa anafanya kazi yake kwa mafanikio ya timu. Mourinho akaanza kuhema vizuri sasa.


Lakini siku tisa baadae, mahusiano yao yakaharibika tena. Mourinho alikipongeza kikosi chake katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Valencia katika Copa del Rey, lakini alitoa kauli za kumsema Cristiano kwenye vyombo vya habari na baadae kwenye chumba cha kubadilishia nguo kwa kumwambia "Shut up and run!" mbele ya wachezaji wenzie. Jambo ambalo lilimshangaza raisi wa Real Florentino Perez lakini aliishia kuambia kwamba suala hilo ni la kawaida kwenye chumba hicho.

Ronaldo alihisi kutotendewa haki na Mourinho ukizingatia alikuwa upande wake pale wote walipomgeuka 0 pia amekuwa ndio msaada mkubwa wa timu uwanjani.

"Naamini hapo ndipo mahusiano yaoyalipofikia hatua mbaya zaidi," kipa wa zamani wa Madrid Paco Buyo alisema. "Ronaldo hakuwa na furaha na ukosoaji kutoka kwa Mourinho - kwa sababu alikuwa naafanya kazi kubwa kwa ajili ya manufaa ya klabu - akifunga mabao meng zaidi."

Mourinho baadae alikaririwa akisema mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 hapendi kupokea ushauri wake wa kiufundi. "Wakati nilimpokosoa kiufundi kwa sababu nilihisi angeweza kuongeza ubora zaidi, hakutaka kukubaliana na nilichokisema. Hilo linawezekana kwa sababu tayari anajua sana na kocha hawezi kumwambia chochote cha kumuongezea ubora zaidi...." aliwaambia waandishi wa habari.


Lakini Ronaldo alishindwa kutaja sababu ya kutokuelewana kwao na Ronaldo, chanzo ambacho kilikuwa ni binafsi zaidi kuliko masuala ya kiufundi.

Ronaldo alichukizwa sana namna Mourinho alivymfanyia - siku kadhaa tu baada ya kumtetea kwa nguvu zote. Kwa mujibu wa watu wa karibu wa mshambuliaji huyo waliongea na vyombo vya habari.

Wiki iliyopita huko nchini Marekani kwenye michuano ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi - Mournho ambaye kwa sasa yupo Chelsea alimtupia kijembe kingine Ronaldo kwa kumwambia yeye sio Ronaldo wa ukweli, akimlinganisha na Ronaldo mbrazil.


Lakini mpaka sasa mshambuliaji huyo amegoma kujibu mapigo akisisitiza, "Kuna vitu kwenye maisha havina thamani ya kuviongelea. Mie napenda kufanya mazungumzo yangu zaidi kupitia uwanjani."

Hii ilikuwa siku moja kabla ya mchezo kati ya Real Madrid vs Chelsea - Ronaldo alimjibu Mourinho kupitia mabao yake mawili aliyoifunga Chelsea na kuisadia Madrid kushinda 3-1. s

2 comments:

  1. Huyo ndo Mourinho a.k.a Domo. Uwe na mashine kama CR7 halafu unaleta dharau wkt ndiye aliyembeba kwa 90% na Mourinho kuendelea kuonekana bora?? ngoja tuuone ubora wake kupitia kwa Lukaku na Torres.

    ReplyDelete