Jamal Malinzi na Ramadhani Naseeb wote wamechukua fomu za kugombea uongozi ndani ya TFF |
Wanamichezo
25 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 27 mwaka huu.
Fomu
hizo zilianza kutolewa juzi (Agosti 16 mwaka huu) ambapo wawili
wamechukua nafasi ya Rais na wengine wawili Makamu wa Rais wakati
waliobaki wanaomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda
mbalimbali.
Waliochukua
fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea urais ni Jamal Malinzi na Omari
Musa Nkwarulo wakati umakamu wa rais hadi sasa umewavutia Wallace Karia
na Ramadhan Nassib.
Waliochukua
fomu za ujumbe ni Athuman Kambi, Charles Komba, Davis Mosha, Elias
Mwanjala, Eliud Mvella, Epaphra Swai, Farid Nahdi, Hussein Mwamba, Jumbe
Magati, Kamwanga Tambwe na Khalid Mohamed.
Wengine
ni Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir, Omari Walii, Samwel Nyalla,
Shaffih Dauda, Stanley Lugenge, Twahir Njoki, Vedastus Lufano, Venance
Mwamoto na Wilfred Kidao.
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu aliyechukua fomu mpaka sasa ni Hamad Yahya anayeomba kuteuliwa kugombea nafasi ya uenyekiti.
Fomu za maombi pia zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ambayo ni www.tff.or.tz Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni saa 10 kamili jioni ya Agosti 20 mwaka huu.
Fomu
zikiambatanishwa na risiti ya malipo (receipt) au malipo ya benki
(deposit slip) kupitia akaunti ya TFF namba 01J1019956700 iliyoko CRDB
tawi la Holland House zirejeshwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa mkono au kwa
barua pepe (email) ambayo ni tanfootball@tff.or.tz .
Wakati huo huo Bwana Jamal Malinzi ametangaza kupitia mtandao wa Twitter kwamba kesho atazirudisha fomu za kugombea urais wa TFF.
No comments:
Post a Comment