Search This Blog

Sunday, September 1, 2013

BABA WA ANDER HERRERA ANAYETAKIWA NA MAN UNITED ASEMA ITAKUWA VIGUMU KWA MWANAE KUONDOKA ATHLETIC BILBAO

Baba wa mchezaji wa Athletic Bilbao  Ander Herrera amezungumza na kusema kwamba itakuw vigumu sana kwa mtoto wake kuondoka kwenye klabu hiyo kufuatia tetesi za uhamisho wa kwenda Manchester United.

Bilbao walithibitisha juzi Ijumaa kwamba wamepokea ofa kutoka kwa Red Devils kwa ajili ya kiungo huyo mwenye miaka 24.

Ripoti zinaeleza kwamba United walituma ofa ya £25m - wakati Bilabo wakihitaji kiasi cha £30.75m kumruhusu Herrera aodnoke na baba yake anaamini itakuwa vigumu kwa mwanae kwenda Old Trafford.


Akiongea na Mundo Deportivo, Pedro Herrera alisema: "Ander anafanya vizuri sana kwenye klabu yake ya Bilbao, anajituma. Amepigana sana kuja kwenye klabu hii na vigumu kwake kuhama.

"Nadhani ni uamuzi wa Manchester United, tangu walimpokosa mbadala wa Cesc Fabregas. Wameamua kuchagua kumtafuta mbadala wake na wakafikiria Ander atafaa."
 

 David Moyes alisema katika press conference yake ya Ijumaa kwamba anategemea klabu yake kuwa busy sana katika siku za mwisho za usajili kabla ya dirisha kufungwa na sasa yakiwa yamebaki masaa tu.

No comments:

Post a Comment