Search This Blog

Friday, July 26, 2013

VIDEO: BARCELONA WAMKOSA MRITHI WA LIONEL MESSI KWA KUKATAA KULIPA GHARAMA ZA KUWAHAMISHA WAZAZI WA MCHEZAJI SPAIN


Kupewa nafasi ya kwenda kujiunga na chuo cha soka kinachoongoza duniani kwa kutoa wachezaji bora La Masia cha Barcelona, ni jambo kubwa sana kwa mcheza soka. 
Huku watoto wengi wacheza soka wakiwa na ndoto za kujiunga na chuo hicho kilichozalisha vipaji kama cha Lionel Messi na Andres Iniesta, mtoto wa miaka 12 Cassiano Bouzon amekataa nafasi hiyo adimu ya kujiunga na kituo hicho cha soka na kuamua kujiunga  Flamengo ya nchini kwake Brazil.

Cassiano amepata kufahamika kimataifa akiitwa jina la  the "Next Lionel Messi"  baada ya vipande vya video zake kupata umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Youtube huku kukiwa na taarifa kwamba alipewa nafasi ya kufanya majaribio La Masia kwa wiki tatu
Lakini kwa mujibu wa wa Globoesporte, Barcelona hawakumpa ofa ya kulipia gharama za yeye kuhamia jijini Barcelona kwa pamoja na wazazi wake, hivyo Cassiano, kwa msaada wa baba yake wakaamua kuhamia kwenye klabu ya Flamengo.


No comments:

Post a Comment