Search This Blog

Thursday, July 11, 2013

QATAR KUTUMIA $200 BILLIONI KWA MAANDALIZI YA KOMBE DUNIA 2022 - KUJENGA VIWANJA KAMA CHA BARCA NA VYENYE AIR CONDITION



Kujenga viwanja vyenye air-condition na vyenye uwazi kwa juu katika jangwa ni gharama sana. 
Kampuni ya Deloitte imesema kwamba Qatar itatumia $200 billion katika kipindi cha miaka 10 ijayo wakati ikijiandaa kuandaa 2022 World Cup, the Associated Press imeripoti.
Fedha hizo zitatumika kwenye miundombinu ya usafiri na utalii pamoja na viwanja vipya. Zaidi ya mashabiki 400,000 wanategemewa kwenda kwenye nchi hiyo kwa ajili ya michuano hiyo itakayochukua mwezi mmoja kufanyika.
Wakati michuano hiyo ikipangwa kufanyika kwenye wakati wa kiangazi, joto hupanda kwa kiasi kikubwa sana, Qatar inajipanga kujenga viwanja vyenye air-condition, pamoja na vyenye uwazi kwa juu ambavyo vyote vitakuwa vikitumia umeme wa nguvu za jua. 

1 comment: