Search This Blog

Thursday, July 11, 2013

MFANYA BIASHARA NDOGONDOGO ATANGAZWA MSHINDI WA DROO YA TATU YA WINDA NA USHINDE YA BIA YA SERENGETI

Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde ambaye ni Bi Blanca Mariki, katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jana jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na wadau wengine wa droo hiyo Meneja mauzo  wa Push Mobile Rugambo Rodney(kulia) na Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko (kushoto).

Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo akiongea na mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde kwa njia ya simu, huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahatinasibu Tanzania Emmanuel Ndaki(wa kwanza kushoto), Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko(wa pili kushoto) na Meneja mauzo  wa Push Mobile Rugambo Rodney(kulia), katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam.

Allan Chonjo ambaye ni Meneja wa bia ya Serengeti akiongea na Blanca Mariki(mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde) kwa njia ya simu katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jana jijini Dar es Salaam. 

Akitoa maelezo kwa wana habari kuhusiana na droo ya tatu ya Winda na Ushinde Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo akiwa na wadau wengine walioshiriki katika droo hiyo jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment