Search This Blog

Thursday, July 11, 2013

MAN UNITED NJIANI KUMPOTEZA THIAGO ALCANTARA: PEP GUARDIOLA ATHIBITISHA KUMTAKA

MANCHESTER UNITED wapo njiani kupoteza nafasi ya kumsaini mchezaji wa Barcelona Thiago Alcantara baada ya kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola kusema kwamba: “Namtaka Thiago hapa Bayern Munich.”

Kiungo huyo mwenye miaka 22 amekuwa kwenye tetesi za kuhusishwa kujiunga na United kwa muda mrefu sasa.
Lakini sasa anaweza akabadili mawazo na kwenda kujiunga na kocha ambaye alimtambulisha kwenye soka la kimataifa wakati akiwa na Barca.
Guardiola alisema: “Namataka Thiago Alcantara. Nimewaambia Bayern wafanye kila kitu kumsajili lakini sijui nini kitatokea.
“Thiago ni mchezaji pekee ninayemhitaji, hilo ndilo nililowaambia.
“Nimsajili yeye au nisisajili kabisa. Tuna wachezaji wengi lakini tunahitaji ubora wa ziada ambao Thiago Alcantara atauleta.
“Namfahamu Thiago vizuri sana. Nimeongea na mwenyekiti Rummenigge na mkurugenzi wa ufundi Sammer kuhusu kumsajili, sasa tusubiri tuone nini kitatokea.
“Sidhani kuongeza kiungo mwingine kutaleta tatizo kwetu. Nimeongea na klabu kuhusu mpango/wazo wangu na sababu za kumhitaji Thiago.
“Nimewapa mawazo yangu, ;alini naisikiliza bodi itasemaje. Wakikataa pia ni sawa.”

1 comment:

  1. uangalie spelling kabla haujapost kaka....otherwise unatupa raha sana ....big up.

    ReplyDelete