Search This Blog

Saturday, July 13, 2013

LIVE MATCH CENTRE: TANZANIA 0 - 1 UGANDA (CHAN 2013) FULL TIME



Dk 90+5 FULL TIME! Taifa Stars 0-1 Uganda

Dk 90 mpira umeongezwa dakika 5. Taifa Stars 0-1 Uganda

Dk 87 Kiungo wa Uganda Kalanda anaumia na wakati huohuo Uganda inapata kona.

Dk 84 Iguma Dennis anamchezea faulo Mrisho Ngassa. Aggrey Morris anapiga faulo juu ya lango la Uganda. Taifa Stars 0-1 Uganda

Dk 81 YELLOW CARD! Majegwa Brian wa Uganda anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kubishana na mwamuzi akipinga filimbi ya kumchezea faulo Bocco.

Dakika 79: Amri Kiemba anapoteza nafasi ya wazi ya kusawazisha akiwa amebaki yeye na mlinda lango 

Dk 79 Kelvin Yondani wa Taifa Stars anaokoa mpira wa hatari uliokuwa unaelekea katika lango la timu yale na mpira unakuwa kona ambayo inapigwa kisha inaokolewa na mabeki wa Taifa Stars.

Dk 76 Mchezo unaendelea na tayari wachezaji wawili wa Taifa Stars ambao ni Athuman Idd Chuji na Khamis Mcha wanapasha misuli moto.

Dk 75 Kabugo Savio wa Uganda anagalagala chini baada ya kuumia na mwamuzi  anasimamisha mchezo ili Kabugo atibiwe.

Dk 74. SUB; Uganda inafanya mabadiliko anatoka Edema Patrick anaingia Ntege Ivan

Dk 71 Ngassa anaisumbua ngome ya Uganda lakini David Luhende anashindwa kuuwahi mpira anaopigiwa na Ngassa.

Dk 63 SUB; Taifa Stars inafanya mabadiliko ametoka Mwinyi Kazimoto ameingia Haruna Chanongo.

Dk 56 Mpira unapasuka baada ya Bocco kupiga mpira na beki wa Uganda akataka kuuzuia.

Dk 54 timu zinashambuliana kwa zamu. Kiungo cha Taifa Stars kinazidi kupwaya.

Dk 46 GOOOOOO....! Iguma Dennis anaipatia Uganda bao la kwanza! Taifa Stars 0-1 Uganda

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA

Dk 45 + 2 HALF TIME! Taifa Stars 0-0 Uganda.

Dk 43 Uganda wanakosa bao la wazi baada ya kuichambua ngome ya Taifa Stars lakini kipa Juma Kaseja anaudaka mpira uliopigwa na Kalanda.

Dk 41 Aggrey Morris anamchezea rafu Kalanda Frank.

Dk 38 Taifa Stars inapata kona. Kona inapigwa na inaokolewa na mabeki wa Uganda lakini kipa wa Uganda Muwonge Hamza anaumia na mpira unasimama kwa muda.

Dk 37 Mpande Joseph wa Uganda anakosa bao la wazi akishindwa kuunga pasi ya Kalanda Frank.

Dk 36 Uganda inapata kona! Inapigwa lakini Taifa Stars wanaokoa.

Dk 33 Aggrey Morris anapiga faulo safi inayotoka nje kidogo ya lango la Uganda.

Dk 32 Said Kyeyune wa Uganda amemchezea rafu Mwinyi Kazimoto.

Dk 31 YELLOW CARD! Wadada Nico wa Uganda anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Ngassa.

Dk 27 Bocco anachezewa faulo na Kabugo Savio.

Dk 24 Kiungo wa Taifa Stars Amri Kiemba anaonekana amechoka sana na anashindwa kucheza katika kiwango chake cha siku zote.Swaumu inaweza ikawa sababu.

Dk 22 Mrisho Ngassa anaiwahi pasi nzuri ya Mwinyi Kazimoto na kupiga shuti kali langoni kwa Uganda lakini mpira unatoka nje.

Dk 20 Bocco anakosa mabao mawili ya wazi katika lango la Uganda baada ya kukosa umakini. Taifa Stars 0-0 Uganda

Dk 19 Aggrey Morris wa Taifa Stars anafanyiwa madhambi na Edema Patrick
.Dk 16 SUB: Uganda wanafanya mabadiliko ametoka Odur Tonny ameingia Kalanda Frank.

Dk 15 Viungo wa Taifa Stars wanakosa umakini mbele ya wenzao wa Uganda huku wakipoteza pasi nyingi.

Dk 13 Uganda wanatawala mpira hasa katika kiungo.

Dk 11: Odur Tonny wa Uganda ameumia na mpira unasimama kwa muda ili atibiwe. Odur ameumia nyonga na anaomba kutoka nje.

DK 5: Timu bado zinaendelea kushambuliana zamu kwa zamu. 

 DK 1: Mpira umeanza hapa uwanja wa taifa na timu zikicheza mchezo wa kusomana taratibu kiasi.

VIKOSI VINAVYOANZA LEO

Taifa Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Salum Aboubakari 'Sure Boy', John Bocco, Mrisho Ngassa na Amri Kiemba.


Uganda; Muwonge Hamza, Waswa Hassan, Wadada Nico, Majegwa Brian, Kabugo Savio, Kasaga Richard, Iguma Dennis, Said Kyeyune, Mpande Joseph, Edema Patrick na Odur Tonny

6 comments:

  1. Wanajipotezea mvuto;wanauzi hawa watt mbaya

    ReplyDelete
  2. Kama wewe ni mzungu halafu kazi yako TZ ni kocha wa kandanda! Halafu una hamu saana ya kwenda kwenu mapema.Basi endelea kuwa na matokeo kama hayo hapo! Aaah muda si mrefu utawaelewa waTz, simile hawana!!

    ReplyDelete
  3. We want a coach to beat Uganda let Kim go!

    ReplyDelete
  4. KUNA SIKU BAADA YA KUFUNGWA NA IVORY COAST NILISEMA TIMU IVUNJWE IBAKI NA VIJANA WACHACHE..........WAJE WENGINE.......SIKUSIKIA MTU ANACHANGIA SASA NADHANI TUMEONA...MATOKEO NI KIWANGO CHA HALI YA CHINI TULIONYESHA MECHI NA UGANDA ISVYO WALITUZIDI KILA IDARA......MFANO MUZRI NADHANI TULIONA JINSI LUEHENDE ALIVYOCHEZA SO TUNGEKUWA NA WAPYA KAMA SITA WANGEJITUMA......WALE WACHEZAJI WATITUMIA NGUVU NYINGI ANA KWA MOROKO NA IVORY COST.......

    TUOMBE MUNGU KUWAFUNGA UGANDA KWAO........!!

    WALE WACHEZAJI WALIO WENGI MICHO ANAWAFAHAMU SO KUTUWIN ILIKUWA NI KAZI RAHISI...BINAFSI HUWA SIAMINI KAMA JOHN BOKO NI STRAIKA WA KUTUKOMBOA....STARAIKA ANAYEZIKAMIA SIMBA NA YANGA.......!!

    ReplyDelete
  5. Hayo ni matokeo ya mpira kuna kufungwa,sare na kushi. Timu yetu ijipange tu tutaitoa Uganda kwa kuwapiga zaidi ya gori mbili. Ushauri wangu ni kuwa wachezaji wa stars wanatakiwa kujengwa Kisaikolojia kwani baada ya kupoteza nafasi ya kupata nafasi ya kuingia mtoano wa World Cup wanaonekana morali yao imeshuka, Ni kazi ya bench la ufundi kukaa na wachezaji ili kuwarudisha katika morali yao na watashinda naamini. Pia kocha aangalie nafasi ya beki na arekebishe upangaji wake. Kwa upande wangu KAPOMBE apangwe beki ya kulia na DAVID LUHENDE acheze beki ya kushoto na pia mbele ya AGREY MORRIS na YONDANI aanze ATHUMANI CHUJI, DOMAYO na SURE BOY striking wacheze BOCCO, KIEMBA na NGASA yaani timu icheze mfumo wa 4.3.3 ambapo Ngasa anatanua kulia na Kiemba anatanua kushoto. Tutashinda kiraisi mchezo wa marudiano. BY MKINGA C.J wa Kimara DSM(a.k.a KOCHA )

    ReplyDelete