Search This Blog

Wednesday, July 3, 2013

CRISTIANO RONALDO: "BADO NAIPENDA MAN UNITED, INGAWA KWASASA NINA FURAHA KUWEPO LA LIGA - ILA SIJUI NINI KITATOKEA MBELENI"

CRISTIANO RONALDO amesema kwamba anamiss sana soka la Uingereza - huku akisisitiza kwamba anafuarahia kucheza kwenye La Liga.

Klabu yake ya zamani Manchester United chini ya boss mpya David Moyes inasemekana wapo kwenye jitihada za kutaka kumrudisha mreno huyo Old Trafford, lakini mshambuliaji huyo wa kireno amekiri kwamba bado anaipenda Manchester United.


“Nimemiss sana soka la England. Kwangu, kucheza pale ilikuwa ni muda mzuri zaidi kwenye maisha yangu ya soka, kila mtu anajua hilo. Manchester United ni klabu ambayo ipo ndani ya moyo wangu. Naimisi sana. Lakini kwa sasa maisha yangu yapo Spain. “Nina furahia kucheza katika La Liga lakini huwezi kujua nini kitatokea huko mbeleni, ila kwa sasa nina furahia kucheza kwenye ligi ya Hispania”
Akiongea katika mkutano ulioandaliwa na Singapore Olympic Foundation, Ronaldo aliulizwa kuhusu Man United na wanafunzi wa Crest Secondary School.
Walipomuuliza kuhusu usajili wa mbrazil Neymar kujiunga na Barcelona, Ronaldo alijibu: “Barcelona wana timu nzuri lakini mie ninachezea Real Madrid, timu bora duniani.
“Ninacheza na wachezaji wazuri mno hivyo kwangu mie haijalishi nini Barcelona wanafanya. Ninachojaribu na kuweka umakini kuichezea timu yangu ya Real Madrid.”

No comments:

Post a Comment