Search This Blog

Wednesday, June 5, 2013

MAKALA: NI UPUUZI KUMSHUSHA THAMANI, KUMUACHA JUMA KASEJA - SIMBA IIGE MFANO WA YANGA KWA NSAJIGWA - MAN U NA GIGGS





KLABU ya soka ya Simba haikuweza kufanya vizuri msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kwani kutoka bingwa mtetezi iliambulia nafasi ya tatu msimu uliopita na kuiacha Yanga ikitwaa ubingwa. 

Hadi kutwaa nafasi ya tatu, Simba ilipambana vilivyo kwani Kagera Sugar nayo ilikuwa ikiwania nafasi hiyo kwa udi na uvumba. Jitihada za wachezaji na benchi la ufundi ndizo zilizoifanya Simba kutwaa nafasi ya tatu.

Usajili ukiwa unaendelea, Simba imeshamsajili kipa Andrew Ntala kutoka Kagera Sugar, huku tayari ikiwa na makipa Juma Kaseja na Abel Dhaira. Usisahau yule wa kikosi cha pili cha timu hiyo.

Wakati Simba ikilundika makipa hao, mkongwe Kaseja ni kama hatakiwi tena na timu hiyo, kwani kitendo cha kumsajili kipa namba moja wa Kagera, Ntala huku Dhaira akiwepo kikosini inaonyesha wazi mmoja kati ya Kaseja au Dhaira anatakiwa kuondoka.
Dhaira hadi anatua Simba alikuwa kipa wa kutegemewa wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, hata huyu Ntala naye ni tegemeo la Kagera. Hii ina maana wote hao sasa wanatakiwa kupambana na Kaseja kuwania nafasi ya kwanza kikosini.

Ni ngumu kwa Simba kuachana na Dhaira kwani mkataba wake ni mkubwa na ambao unaweza kuigharimu Simba kiasi kikubwa cha fedha kuuvunja.
Popote pale duniani, huwezi kusajili makipa namba moja wawili kutoka timu nyingine huku tayari ukiwa na kipa hodari. Hii ni sawa na usajili mwingine wa nafasi nyingine uwanjani.
Tayari kuna tetesi kwamba, Simba ipo tayari kumwachia Kaseja ajiunge na klabu nyingine kwa madai ya kushuka kiwango na kushindwa kuisaidia timu kushika moja kati ya nafasi mbili za juu.
Mchakato mzima wa kuhakikisha Kaseja anaondoka Simba unaongozwa na kiongozi mmoja ambaye sasa ana sauti ndani ya klabu hiyo na mbaya zaidi hakuna sababu za msingi za kumuacha Kaseja.

KUSHINDWA KUISAIDIA SIMBA
Sababu kwamba Kaseja ameshindwa kuisaidia Simba haingii akilini kutokana na ukweli kwamba hata katika mechi ambazo Simba imefungwa Kaseja akiwa langoni, kuna vitu vingi vilikuwa vinatokea.
Hadi sasa hakuna hoja ya msingi iliyotolewa na uongozi juu ya mpango huo unaotengenezwa wa kuhakikisha Kaseja anaondoka Simba kwa njia yoyote ile, bali inayolazimishwa ni hii ya kushindwa kuisaidia timu.
Hawafafanui jinsi kipa huyu alivyoshindwa kuisaidia Simba kushika moja kati ya nafasi mbili za juu, kwani hajawahi kufungwa mabao manne katika mechi moja na idadi kubwa ya kufungwa kwake katika mchezo mmoja haizidi mabao matatu.

HAKUWA NA WASAIDIZI WA MAANA

Ikumbukwe ya kwamba, Kaseja ni kipa imara anapokuwa na mabeki imara, sasa tazama ndani ya msimu huu alikuwa na mabeki wa kati wa aina ipi na walikuwa na uwezo upi.
Msimu wa 2011/12 ambao Simba ilitwaa ubingwa, kwa kiasi kikubwa Kaseja alilindwa na mabeki Juma Nyosso na Kelvin Yondani, hao aliweza kuwapanga ipasavyo na ni safu iliyokuwa ikielewana kwa muda mrefu.
Msimu uliopita Kaseja amecheza na safu nyingi za ulinzi wa kati Victor Costa, Nyosso, Shomari Kapombe, Komalbil Keita, Pascal Ochieng, Mussa Mudde hadi chipukizi Hassan Khatib. Tazama mlolongo huo wa mabeki.
Utitiri huo wa mabeki haukuweza kumsaidia Kaseja kwani ulikuwa ukibadilika kila mara na mwisho wake hata kocha Patrick Liewig akawa anafanya kazi ya kujaribu mabeki hadi ligi inaisha.
Tazama kiungo Mudde aliyesajiliwa katika timu kama kiungo lakini kutokana na uhaba wa mabeki, Simba ikaamua kumchezesha kama beki. Mbaya zaidi akachezeshwa katika nafasi hiyo kwenye mechi muhimu kama ya Simba na Yanga.

KASEJA ANAFUNDISHWA NA NANI?


Unaweza ukaona kama utani lakini ndiyo soka lilivyo, kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ wa Yanga aliichezea Simba msimu wa 2011/12, hakuwa akipata nafasi na hata alipopewa nafasi alikuwa hafanyi vizuri kama ilivyo kwa Kaseja, ili lipo wazi.
Lakini msimu uliopita, Barthez aliipa Yanga ubingwa na kutangazwa kuwa kipa bora wa ligi nzima. Sababu zipo wazi.
Akiwa Simba, Barthez alikuwa anapata mafunzo ya ugolikipa akiwa sambamba na Kaseja, lakini alipotua Yanga ndani ya muda mfupi timu hiyo ikampa kazi Razack Siwa, ambaye pia ni kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.
Siwa ni kipa wa zamani pia aliwahi kuinoa Yanga tena kwa nafasi zote mbili, kocha mkuu na kocha wa makipa, kwa kifupi huyu amesheheni katika kufundisha makipa na ameshasoma kozi kibao za kufundisha makipa.
Katika mahojiano na kituo cha runinga cha Clouds kupitia kipindi cha Sports Bar, Siwa aliwahi kusema tatizo la wakufunzi wengi wa makipa, wanafanya mambo ambayo hayatokei uwanjani na wanashindwa kumuandaa kipa kuwa jasiri uwanjani.
Anatolea mfano kwa mazoezi ya kuwarushia mipira makipa ili wadake, Siwa anasema hilo ni tatizo kwani kipa akiwa uwanjani anapigiwa mashuti na wala harushiwi mipira na wachezaji wa timu pinzani. Siwa huwapigia mashuti makali makipa wake katika mazoezi.
Huo ni mfano mdogo tu wa Siwa, lakini kuna vitu vingi ambavyo vinamfanya Barthez aonekane anafanya vizuri uwanjani, lakini bado huyu ni yuleyule na Kaseja ni yule yule.
Barthez msimu wote huu amecheza chini ya mabeki Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na wakati mwingine Athuman Idd Chuji au Mbuyu Twite. Hao wote ni wachezaji wazoefu. Hata hivyo muda mwingi walicheza Cannavaro na Yondani.

POULSEN ANAWAKOSOA
Pamoja na Simba kumuona wa nini, bado Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen anamuona Kaseja ni kipa bora na ndiyo maana anaendelea kumuita kikosini na kumtumia pia.
Poulsen siyo kwamba haoni vipaji vya makipa Mwadini Ally wa Azam FC na Barthez, kuna kitu cha ziada anachohitaji kutoka kwa Kaseja ndiyo maana anamtumia kikosini.
Kitu ambacho Poulsen amekiona kwa Kaseja ni uzoefu ambao haupo kwa Barthez au Mwadini japokuwa wote wana viwango vinavyolingana.

SIMBA HAITAKI KUWA NA GIGGS WAO?
Ukongwe ndani ya timu ya soka ni moja kati ya vitu muhimu ambavyo klabu nyingi za Ulaya na Afrika vinahitaji ili kuzifanya ziwe na maendeleo.
Kaseja ameichezea Simba kwa zaidi ya miaka 10 sasa, maana tangu ajiunge nayo mwaka 2002 akitokea Moro United ameachana nayo mwaka mmoja tu alipotimkia Yanga.
Manchester United inapohakikisha inabaki na mtu kama Ryan Giggs kikosini huwa inahitaji maendeleo kwani damu changa peke yake si rahisi kuipa mafanikio. Wakongwe ndiyo wanaotumiwa kuweka mambo sawa kati ya uongozi na klabu.
Yawezekana Simba sasa inamuona Kaseja kama kikwazo cha wao kuwamiliki na kuwatumikisha itakavyo wachezaji chipukizi tena kwa malipo hafifu, maana yawezekana wanamuona Kaseja atawafuta mchanga machoni.

HAWAONI YALIYOTOKEA KWA CASILLAS & MOURINHO  
Ni ukweli usiofichika kwamba, kipa Iker Casillas ndiye kila kitu kati ya wachezaji wa Real Madrid na hata timu ya taifa ya Hispania. Kocha Jose Mourinho muda mfupi baada ya kutua kuifundisha klabu hiyo alitaka kufuta hali hiyo kwa Casillas.
Mourinho alitaka yeye kuwa mtu muhimu katika timu kuliko Casillas, akamtengezea mazingira kipa huyo ya kuonekana hafai na kuanza kumuweka benchi bila sababu ya msingi.
Hata hivyo, Madrid ni miongoni mwa klabu zinazothamini mchango wa wakongwe kama Casillas ambao wanaweza kuisaidia timu ndani na nje ya uwanja. Ikaamua kuachana na Mourinho ili ibaki na Casillas.
Ndiyo maana Chelsea leo hii ina John Terry, Liverpool yupo Steven Gerrard, Man United wanaye Giggs, na hata Yanga wanaye Shadrack Nsajigwa. Sasa iweje Simba imtimue Kaseja?
Umefika wakati sasa siasa na chuki zisizo na maana ziondoke katika mazingira ya soka letu ili tuweze kufikia mafanikio.

11 comments:

  1. Wakati mwingine nyie waandishi mnaojifanya mnaweza kuandika makala mnachemsha sana! Kwa sababu Simba ni nani mpaka mtake kila mwaka iwe yenyewe tu inachukua ubingwa! Hata kwa man U uingereza na Real madrid hispania haijawahi kutokea hivyo.Hakuna ubishi kuwa Kaseja ndiye golikipa bora zaidi ukanda huu wa Afrika mashariki,lakini hakuna ubaya wowote kwa ujio wa Ntala na Dhaira kwa kuwa inahitajika Simba imara.Tumeona Kaseja akicheza mfululizo kwenye Timu za Taifa na Simba kufikia na yeye kuchoka kama binadamu.Sasa hata kipindi hicho bado Simba itahitaji golikipa imara kama Kaseja!! Lakini mwandishi wewe unadai hilo ni sawa na kumfukuza Kaseja! Unalitoa wapi?Pale Simba kuna Kocha Kisaka! Ana historia ndefu na uzoefu we humuoni!!umemwona Siwa, Ebu tutolee uyanga wako hapo!Siku ingine ukijiona unataka kulete makala kaa chini kwanza utulize akili!!

    ReplyDelete
  2. Matatizo ya fani muhimu kuisomea kwa miezi mitatu!!

    ReplyDelete
  3. labda mimi ninachokiona kwenye hii makala ni kutaka kumtengenezea mazingira kaseja ili apige mawe ndani ya simba,kaseja wa leo sio wa miaka mitatu nyuma lazima ukubari shaffih,angalia magoli ya kijinga anayofungwa now days mfano magoli aliyofungwa na libolo yalikuwa ya kijinga zaidi kaseja kuwahi kufungwa,kaseja wa sasa sio mcheza cross kama kaseja wa zamani dats means uwezo wake umeanza kupungua kwa kujiona hakuna kama yeye,tuliona alivyofungwa na moroko goli la cross akaja akafungwa tena na yanga goli la cross,kama kweli kaseja ni kipa bora asajiliwe na azam ama yanga ama mtibwa or coast staki kuamini kuwa hakuna kama kaseja bongo hata sharifu wa mtibwa pia yuko vizuri kaka

    ReplyDelete
  4. Kwngu mm ww mwandish nakuona ni mnafiki na mchonganish kwn kaseja ni nani hasa pale simba mbona babu pale man u,alimuuza becks na dunian kote kwa sasa soka wanawekeza kwa vijana sasa mbna inakuuma simba kuwapa mikataba chipukizi!mpka unafikia hatua ya kusema wanawapunja kua fea mwandish ww ni kioo cha jamii bwna,unakumbuka kama kaseja aliisaliti simba na kwenda yanga?vp unataka kumfananisha na m2 kama steve G au Giggs ambao maisha yao ni klabu moja 2 bac kama kaseja ni mzuri kuliko makipa wote bac anzisha timu yako umchukue waache simba wafanye mambo yao bana.!

    ReplyDelete
  5. huo ni mtazamo wko tu mwandish ila ukweli upo wazi cyo kila mchezaji anaeachwa kuwa kiwango kimeisha wengine wanaachwa kwa sababu ya majungu kwenye timu,nyinyi ndyo mnaopanga timu wakati mwalimu yupo wewe ni mwandishi tu huna elimu yoyote kuhusu mambo ya ukocha,marcimo alikuwa hamtaki kaseja timu ya taifa na alisema cyo kwa sababu ya kiwango ila alisema cyo mzalendo tujaribu kuwa wakweli jamani kwan kaseja ni nani hasa pale simba ina maana kaseja akicha soka simba nayo ife?lingine ina maana kisaka cyo mwalimu mzuri wa makipa?basi anzisha timu yako umchukue kaseja akachezee kwan timu ni simba tu tanzania hii?.

    ReplyDelete
  6. Tatizo letu watanzania huwa hatujibu hoja, huwa tunaanza kumsakama mtoa hoja. Mada iliyojadiliwa ni mtazamo wa mwandishi, na si lazima kila wakati huo mtazamo ufanane na wa kwako, sasa tunafanyaje? unapoona hoja iliyoletwa haina mashiko, andaa makala ambayo itakuwa na mtazamo unaohisi kwa upande wako ndio hoja yenye mashiko, mtumie mwandishi huyohuyo ikiwezekana (ku-pose counter-argument) au tafuta mahala kwingine, chapisha hoja yako, na si kuanza kumponda mtoa hoja.

    Ukianza kumponda mwandishi huku wewe hatujui utendaji wako kwenye hiyo taaluma au ujuzi kazini kwako, hutendi haki, na mara nyingi wasema hovyo makazini kwao ndio huwa watendaji wabovu, lakini huona ya wenzao tu. JIFUNZENI KUJENGA NA KUJADILI HOJA NA SI KUMSAKAMA MTOA HOJA.

    ReplyDelete
  7. Kama suala ni kumjadili mtoa hoja na si mada, WE HAVE A VERY LONG WAY TO GO.

    ReplyDelete
  8. dah! me i guess na agree na the writer coz its true anachosema, u guys mnaodiss i sorta kinda don understand u, the guy who rote this ni expert n he has done his research,

    ReplyDelete
  9. Shafiiih mpenzi mkubwa wa soka la nje ambalo analiona kupitia tv ambayo tukio likitokea linarudiwa( slow motion) hivyo kumuwezesha kurikariri huku akisikiliza kwa makini nn mtangazaji anaelezea kisha jioni kuutangazia umma kwa mbwembwe matokeo ya ulaya na jinsi mpira ulivyochezwa tofauti kubwa kuona tukio mara moja kwenye mpira wa bongo huku likiwa halirudiwi kisha ulielezee kwa kina na kwa ufasaha na wasikilizaji wakuelewe na kuukubali ukweli huo.maana nimeona mara kibao mabao yanafungwa kwa mguu au kichwa taarifa zinakuwa tofauti msomaji au msikilizaji unabaki kuduwaa binafsi nawakumbuka na kuwapongeza watangazaji na waandishi wazamani kama Ahmed Jongo.Seleman Kumchaya. Salim mbonde na wengine bila kuwasahau James Nhende na Jonson mbwambo hakika hamjaacha warithi wenu ktk tasnia zenu maana wengi wanajaribu kuwaiga badala ya kutoka na vipaji vyao halisi maana ya kuandika hivyo ni baada ya kusoma makala hii huku mwandishi akishindwa kutoa ushauri kwa Kaseja afanye nn ktk khali hii huku wakibakia kuomba huruma za viongozi najiuliza hivi hilo soka la ulaya wanaloliabudu na kulitolea mifano halina kipa mahiri ambaye kaseja anapaswa kufuata mifano basi mm namshauri amsome Peter Shmirchael baada ya mafanikio aliamua nn hapa nyumbani Omar Mahadhi aliacha kwenda Brazil ili Moses Mkandawire aende kwa manufaa ya klabu yake.Pondamali Juma akiwa kipa wa kutisha hapa bongo lkn bado aliishi na Idd Msakaa na kumlea huku akimpa mechi muhimu nawakilisha.

    ReplyDelete
  10. Shaffih mimi si muumini wako mara nyingi nimekuwa nikikupinga lakini kwa hil la leo mimi nakuunga kono uko sawa sawa kabisa na sasa umewaona wana Simba hawa walivyo wana chuki na Juma kama ilivyokuwa kwa viongozi wao,Juma ndiyo kipa bora kuliko wote na hata wao wenyewe wanamjua Juma ni nani katika mioyo yao,Kuna viongozi wana chuki kubwa sana na Juma na wanataka kuhakikisha kuwa wana mtoa kwa gharama yeyote ile na ushahidi tunao ninawapa:-walimwambia Phiri asimpange kule eti Jumaa anafungsha Phiri aligoma akafukuzwa yeye,walimwambia Milovan asimpange eti anafungisha unajua kilichomtokea tusirudie,mekuja mfaransa viongozi wakatangaza kumvua unahodha awe Shomari,lakini wakamsingizia mwl mpya anataka kuchagua nahodha wake,mwl akawaaibisha viongozi akamchagua nahodha wake Juma K Juma,kana kwamba haitoshi a hata kipa chaguo lake la kwanza likawa Juma na hata siku ya mechi ya imb na Yanga walipomtaka Dhaira ndiyo adake na Ngassa asicheze bado alwakatalia na ameishatupiwa virago wamemleta mwalimu King ambaea atakuwa tayari upokea vimemo nani acheze na nani asichze,sasa hata kama Juma kweli amechoka na ndiyo adhalilishwe nanmna hiyo nani asiye jua thamani na mchango waJuma ndani ya Simba achene unafiki nyie oya oya msiyo jua mpira.

    Big up Dauda sana endelea kuwapasha.



















    ReplyDelete
  11. Sijaelewa chochote iko inaload........

    ReplyDelete