Search This Blog

Tuesday, June 25, 2013

KALI YA LEO: MANCHESTER CITY YAPIGA MARUFUKU WAFANYAKAZI WAKE KUVAA JEZI ZA MAN UNITED - WAKIWA KAZINI.

Manchester City wamewapiga marufuku wafanyakazi wake kuvaa jezi za Manchester United wakati wakiwa kazini. 

The Mirror inaripoti kwamba wafanyakazi wanaofanya kazi ya ujenzi wa kituo kipya cha kambi ya Man City - Etihad chenye thamani ya £120million wameonywa kwamba watafuuzwa ikiwa watakuja kazini wakiwa kwenye uzi mwekundu wa United.

Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja anayefanya kazi kwenye eneo hilo la ujenzi amesema jezi za timu nyingine zote zimepigwa marufuku kuonekana zimevaliwa kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na uwanja mpya wa mazoezi wa City. 

Hatua hii imekuja baada ya tukio lilotokea wiki iliyopita ambapo wajenzi wawili wapenzi wa United walikwenda site wakiwa wamevalia jezi za United na hivyo wakaambiwa wavue jezi ndio waendelee na kazi.


No comments:

Post a Comment