Search This Blog

Monday, June 17, 2013

BAADA YA KUIKOSA SAFARI YA BRAZIL 2014 - TAIFA STARS SASA KUINGIA KAMBINI JULAI 4 - SAMATTA NA ULIMWENGU WATEMWA

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kim amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.

Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Mechi hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

5 comments:

  1. Shafii huwezi andika Samata na Ulimwengu wametemwa ila hayo mashindano hayawahusu.

    ReplyDelete
  2. mbona magolkipa kibao?

    ReplyDelete
  3. watu wa blog hii sijui wamesomea uandishi habari chuo gani mashindano ya CHAN hushirikisha wachezaji wa ligi ya ndani ya nchi(local)unapokuja na kichwa cha habari samatta na ulimwengu watemwa sikuelewi.

    ReplyDelete
  4. Huyu kocha awe anasikiliza maoni na ushauri.Ni kweli kikosi cha Uganda kitakachocheza CHAN kitakosa karibu mastaa 10 wa first eleven wanaocheza nje ya nchi hiyo,lakini wenzetu wako makini sana kwenye kutumia makosa au udhaifu wa wapinzani.Erasto Nyoni ni beki mzuri kwa vigezo vya nafasi hiyo lakini anahitaji kuwa na msaidizi wa uhakika iwapo lolote litatokea,lakini sidhani kama Vincent Barnabas ndiye mtu sahihin kwa jukumu hilo,kwani ana umri mkubwa,kimo kifupi na hajacheza nafasi hiyo au nafasi yoyote ya beki katika klabu zote alizochezea ligi kuu kuanzia 2005.Magoli matano kati ya sita ambayo Stars imefungwa katika mechi mbili zilizopita yalitengenezwa kutokea pembeni.Hivi Cholo au Michael Pius wanazidiwa uwezo na Barnabas katika nafasi ya beki wa kulia?Halafu anapaswa kumpa nafasi Kiemba ya kupiga baadhi ya mipira ya adhabu ndogo kwa kuwa anatumia akili sana na ana shabaha.Najua kuna watu watadai ninaingilia kazi ya kocha ambaye ni professional lakini tukumbuke kwamba ile oparesheni ya kichwa aliyofanyiwa mgonjwa mwenye tatizo la goti ilifanywa na profeshno na pia haya magorofa yanayoporomoka kila kukicha yanajengwa na maprofesho wasiotaka kushauriwa

    ReplyDelete
  5. Shaffi huu sio uandishi murua kaka hawa hawajatemwa bali mashindano yajayo ni ya wachezaji wa ligi za ndani. Kwa nini waandishi mnaandika irresponsibly namna hii uandishi wa habari kama huu hautakubalika kamwe . TUTAKE RADHI WADAU WA SOKA KWA ROHO SAFI.

    ReplyDelete