Search This Blog

Sunday, May 5, 2013

JUVE YATWAA TENA UBINGWA WA SERIE A.

Beki Giorgio Chiellini amebeba bango linalomaanisha ubingwa wa 31 wa Juve - ukiwemo mara mbili waliovuliwa kutokana na kashfa ya upangaji matokeo.



Juventus imefanikiwa kuchukua ubingwa wa Serie A kwa mara ya 29 kutokana na ushindi finyu leo hii kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Palermo.
Bao la mkwaju wa penati lililofungwa kipindi cha pili na kiungo Arturo Vidal lilitosha kuwapatia Juve ushindi wa bao 1:0 na kujihakikishia ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo huku ikiwa imebakia michezo mitatu,pia kwenye mchezo huo kiungo wa Juve Paul Pogba alilimwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtemea mate mchezaji wa Palermo.

No comments:

Post a Comment