Search This Blog

Monday, April 22, 2013

WAKATI LIGI KUU YA TANZANIA IKIWA INAHAHA KUONYESHWA SUPERSPORT - LIGI YA DARAJA LA KWANZA KENYA KUANZA KUONYESHWA NA SUPERSPORT

Jack Oguda, Auka Gecheo and Sam Nyamweya @ SS com
Wakati ligi kuu ya Tanzania ikiwa haionyeshwi hata vituo vya nyumbani - Kituo cha televison cha SuperSport wanatarajiwa kuanza kuonyesha mechi kadhaa za michuano ya FA/ligi ya daraja la kwanza Kenya iliyo chini ya shirikisho la soka la nchi hiyo. 

Hatua hii inakuja baada ya mkataba baina ya kituo hicho cha Televison cha Afrika ya kusini, ambao pia wana mkataba wa kuonyesha ligi kuu ya Kenya iliyo chini ya Kenyan Premier League, na sasa wataanza kuonyesha mashindano ya pili kwa ukubwa nchini humo. 

"Tuna furaha kwa ushirikiano huu na FKF na kupata nafasi ya kuonyesha ligi ya daraja la kwanza. Hatua hii inaonyesha namna tunavyothamini maendeleo ya soka ndani nchi hii na kutupa nafasi nzuri ya kuwa sehemu ya mfumo mzuri wa utawala mpya wa soka nchini Kenya," alisema mkurugenzi mkuu wa SuperSport East Africa Auka Gacheo.

Kufuatia dili hii ligi ya daraja la kwanza Kenya, inakuwa ligi ya daraja la kwanza y pili kuonyeshwa barani Afrika na SuperSport ikiifuatia ligi ya daraja la kwanza ya Afrika ya Kusini.

2 comments:

  1. SASA SHAFII HEBU TAFUTA INTERVIEW NA MWAKILISHI WA SUPER SPORTS KWENYE UKANDA HUU NADHANI UNAWEZA KUISAIDIA JAMII ZAIDI. HAPA KUNA TATIZO TENA KUBWA SANA. HEBU MTAFUTE HARAKA KAMA ATAPENDA KUZUNGUMZIA HILI SUALA LA MASLAHI.. MIMI HIZI SINEMA ZA VIONGOZI WA BONGO ZIMENICHOSHA.

    Mtanzania X

    ReplyDelete
  2. hongera shafii kwa kutupa habari za kujenga an siyo habari za migogoro kila kukicha.Tatizo lilipo hapa kwetu ni upeo mdogo wa viongozi husika kwenye masuala yote ya uendeshaji mpira pia mgongongano wa maslahi!!(nitanufaika vipi).

    Shafii fanya mchakato wa kumpata mwakilishi wa supersport ili atupe maoni yake nini kifanyike tutoke gizani.

    ReplyDelete