KOCHA Mkuu wa Simba Patrick Liewig ameweka wazi mipango yake ya usajili kwa ajili
ya msimu ujao wa ligi na tayari amepanga kusajili wachezaji watano wapya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.Mfaransa huyo alisema kuwa anaamini kuwa akitupa karata zake vyema kwenye usajili bila shaka Simba msimu ujao utakuwa vizuri.
“Msimu ukimalizika nina mpango wa kusajili wachezaji watano ambao kwa kipindi hichi nimewatazama na ninaona kuwa wanaendana na matakwa ya kikosi changu kuanzia nidhamu hadi uwezo."
“Tumekaa na wenzangu wa benchi la ufundi lakini bado hatuja hamua yupi wa kumchukua na kumwacha, kwani kwa kawaida ni wachezaji wa kutazama zaidi kwa sababu ni suala ambalo linahitaji utulivu mwingi na umakini wa hali ya juu."
“Nadhani kwa mtazamo wangu na makubaliano na benchi la ufundi, naona kuwa tutasajili watano ambapo kati yao wawili watakuwa ni wa nafasi ya ulinzi, kiungo mmoja na washambuliaji wawili."
Kocha huyo amekuwa akieleza mara kwa mara kuwa anatarajia kubadilisha hali za wachezaji na kuwawezesha kuonesha kiwango kizuri ili kulingana na dhamani ya pesa wanazochukua kwenye klabu hiyo.
“katika usajili wangu, natarajia kuwachukua wachezaji wawili wa kimataifa, wakati wengine watatu watakuwa ni wa hapa nyumbani Tanzania na kushirikiana na yosso waliopo,” alisema kocha huyo.
Yosso waliotokea Simba B ambao Liewig amekuwa akiwatumia kwenye michezo ya ligi ni pamoja na mabeki Miraji Adam na Hassan Khatib, viungo Abdallah Seseme na Said Ndemla na winga Haroun Athuman 'Chanongo' wakati upande wa ushambuliaji ni Rashid Mkoko.
Wazoefu waliopo kwenye kikosi hicho ni Juma kaseja, Nassoro ‘Chollo’, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa na Shomari Kapombe.

No comments:
Post a Comment