Search This Blog

Friday, April 5, 2013

BAADA YA KUWACHINJA WABOTSWANA KWAO - SAMATTA SASA KUIVUSHA MAZEMBE JUMAPILI MABINGWA WA AFRIKA?


TP Mazembe watawakaribisha Mochudi Centre Chiefs jijini Lubumbashi hapo Jumapili huku macho yote yakiwa kwa mshambuliaji Mbwana Samata kuwavusha kuingia raundi ya pili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania ameuanza vizuri mwaka 2013 katika klabu na timu ya taifa baada ya kufunga mabao matatu katika michezo miwili aliyocheza hivi karibuni.
 

Samata amereja Mazembe akiwa na hali kubwa baada ya kufunga mabao mawili kwa Taifa Stars iliyoshinda 3-1 nyumbani dhidi ya Morocco jijini Dar-es-Salaam katika mchezo wa kusaka kufuzu kushiriki Fainali za  Kombe la Dunia 2014.
 

Kiwango chake kimekuwa ni habari njema kwa kocha wa Mazembe, Lamine Ndiaye mwenye matumaini ya kuiongoza timu hiyo ya DR Congo kuibwaga Mochudi katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 

Mazembe kwa sasa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Mochudi ushindi iliyopata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Machi 16 jijini Gaborone, ambapo goli hilo pekee lilifungwa na Samata.
 

Pamoja na ukweli kwamba ubora wa Mazembe unamtegemea Samata, kocha wa Mochudi, Madinda Ndlovu bado anaamini kuwa kikosi chake kitafanya maajabu Lubumbashi hapo Jumapili.
 

"Bado hatujakata tamaa pamoja na kuwa tumefunga bao moja nyumbani kwetu,” alisema Ndlovu.
Wakati huo huo; hakuna timu iliyowahi kuifunga Mazembe jijini Lubumbashi kwa zaidi ya miaka kumi sasa katika mashindano haya ya Afrika.

No comments:

Post a Comment