Search This Blog

Thursday, April 11, 2013

AZAM IWASAFISHE NA IKIWEZEKANA IWALIPE FIDIA KINA MORRIS, NYONI, MORAD NA DIDA…

SIKU chache baada ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Bara dhidi ya Simba uliochezwa Oktoba mwaka jana, Azam FC ilitangaza kuwasimamisha wachezaji wake wanne kwa tuhuma za kuuza mechi hiyo, sasa wachezaji hao wameonekana hawana hatia, hivyo klabu hiyo inapaswa kuwalipa fidia kwa kuwadhalilisha.

Wachezaji Erasto Nyoni, Said Morad, Deo Munishi ‘Dida’ na nahodha Aggrey Morris, ndiyo waliotuhumiwa kupokea fedha kutoka Simba ili wacheze chini ya kiwango na kufungwa mabao 3-1. Azam ilienda mbali zaidi baada ya kulifikisha jambo hilo kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) ili kubaini ukweli wa mambo na watuhumiwa kuadhibiwa.

Wachezaji hao waliondolewa katika kikosi cha Azam na wengine wenye bahati walikuwa wakiichezea timua ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kila mara hadi hivi karibuni walipoichezea timu hiyo dhidi ya Morocco na kuifunga mabao 3-1.

Wachezaji hao ni Morris na Nyoni. Tangu mwaka jana waliposimamishwa hadi ‘walipofutiwa mashtaka’ juzi, inaelezwa wachezaji hao walikuwa wakilipwa stahili zao zote na Azam huku jambo lao likiendelea kuchunguzwa na Takukuru. Hata hivyo, wachezaji wote hao hawakubweteka na badala yake wakawa wanafanya mazoezi na klabu zao za mitaani. Hicho ndicho kilichowasaidia Morris na Nyoni kuendelaa kuitwa kikosi cha Taifa Stars.

KULIPWA KWA WACHEZAJI
Japokuwa Azam ilikuwa ikiwalipa mishahara wachezaji wake iliyowasimamisha, kuna haja ya klabu hiyo kuwalipa fidia wachezaji wake kwani iliwatangaza wenye hatia ya kupokea hongo hivyo kuonekana tofauti katika jamii.
Vyovyote vile, wachezaji hao wanaishi katika jamii, hivyo kitendo cha kutangazwa wanatuhumiwa ‘kuuza’ mechi, kimechafua majina yao.
Hakuna kitu kibaya katika soka kama kashfa ya kupanga matokeo kwani adhabu yake ni kubwa na inahusu muhusika kutojihusisha na mambo ya soka maisha. Kwa kuzingatia hili, Azam inapaswa ‘kuwasafisha’ nyota wake hao na ikiwezekana kuwalipa fidia.


MASWALI BILA MAJIBU

 Azam ilidai ina kila kitu kuhusu ushahidi wa tukio lenyewe, ina maana ushahidi huo haukuiridhisha Takukuru? Je, ni kweli kwamba mambo yameisha kinyemela kwani kama vielelezo vingetumika kama vilivyo kulikuwa na hatari ya Simba kuathirika na hata kushushwa daraja hivyo kupunguza ushindani katika ligi?

1 comment:

  1. hilo ni kweli ila swala la takukuru kutowakuta na hatia ni kawaida coz kuna kesi ambazo mtu amekamatwa on the spot akitoa au kupokea rushwa lakini mwisho wa kesi takukuru wanasema wameshindwa kumkuta na hatia so ivyo ndivyo takukuru wanavyofanya kazi, wakati mwingine mpaka najiuliza sasa kazi yao ni nini na wapo kwa faida gani.

    ReplyDelete