Search This Blog

Wednesday, March 13, 2013

PAMOJA NA KUTOKUWA NA TIMU ERASTO NYONI, AGGREY MORRIS WAITWA STARS - JOHN BOCCO NDANI - TEGETE AENDELEA KUTOSWA


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco.

Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

10 comments:

  1. sasa tuache kuongelea watu na uchaguzi, tujikiti kwenye suala hili muhimu, sina matatizo na timu kwanza ndio ile ile, wako vizuri, tuwape sapoti tu, inawezekana kuwafunga Morocco. kafa cameroon na mabingwa wa afrika zambia hapa. JAMANI NAIPENDA SANA TAIFA STARS, NAOMBA TUSIANZE KUONGELEA MCHEZAJI MMOJA KAMA ULIVYONZA ETI TEGETE KATOSWA. KOCHA AKIONA ANAFAA ATAMWITA MBELENI. TANZANIA GO, GO, GO. SHAFFIH KAPIGENI HAKA KAWIMBO KANANIKUMBUSHA MBALI SANA

    ReplyDelete
  2. Naona jamaa anajitahd ku-maintain kikosi....labda!

    ReplyDelete
  3. KWA STILI HII NAMPONGEZA SANA KOCHA WA TAIFA STARS KWA SABABU HABADILISHI KIKOSI.NI KWELE WAKINA MORIS HAWACHEZI LAKINI KULINGANA NA MFUMO WA MWALIMU WAMESHAUZOEA NDIO MAANA MWALIMU HATAKI KUINGIZA WACHEZAJI WAPYA MAANA ATAANZA UPYA .

    ReplyDelete
  4. Safi sana hapo juu mchangiaji wa kwanza, maana huyu kasema oooh Tegete kaachwa pia kuna mwenzake kaandika Barthez kaachwa, majina ya nini jamani? Yaani mtu ana-mention Barthez out of Kaseja, Mwadini na yule kipa wa Mtibwa Hussein Sharrif, dah tuache hizo jamani au mmeshaanza tena kuhesabu wa SIMBA wako wangapi ili m-balance na wa YANGA?

    ReplyDelete
  5. lakini kwenye benchi la ufundi hakuna mzanzibari hata mmoja hii ni haki na hii ni timu ya nchi mbili hata mtunza vifaa (jezi) basi hawezi kutoka zanzibar. mara nyingine mutuone na sisi tutashtaki (CAS)

    ReplyDelete
  6. Keep it up KIM.. I see what u mean.

    Mchangiaji Anonymous March 13,2013 at 6:50AM. You are absolutely right, labda hii timu ni ya TFF ya Tanganyika tu,

    ...MKATABAA..

    ReplyDelete
  7. duuh ni kweli benchi la ufundi limejaa wabara tff lizingatieni hili

    ReplyDelete
  8. hapa hatutaki shabiki wa Simba wala Yanga, tulia hivyo hivyo ucichangie chochote.
    Hapa tunataka Shabiki wa Taifa star tu.
    Nina imani tutashinda kikubwa ni kwa wachezaji kujua/kutambua wanahitaji nn na si kucheza mpira pekee.

    ReplyDelete
  9. Asante sana Kim.kocha kawaita wachezaje ambao anaona watamsaidia kupata ushindi kulingana na mfumo unaotumika.swala la sijui "nani hajaitwa" halina mantiki hapa. siku zote mashabiki wana expectations zao katika jambo lolote but hapa ufundi ndo unachukua nafasi yake.yani mtu kuibukua tu round ya pili na kufunga hivyo vijimagoli ndo haitwe? TEAM WORK MUHIMU.

    ReplyDelete
  10. Kocha ndio mwalimu na ndio alihetufikisha tulipo. Tisapot timu yetu, ingekua hivyo kila mtu anataja mchezaji wake basi tungekua na timu ya Taifa ya wachezaji 40. Tusapoti timu, kila mtu ajitahidi kupata hata marafiki ama jamaa watatu aje nao uwanjani hata kama hawatavaa jezi ya Stars lakini uwepo wao bado ni sapoti sana kwe Timu!
    Moroco HAWACHOKI kwetu. Kwa fitna zote.
    Asante.

    ReplyDelete