WACHEZAJI wa Simba waliokuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kilichocheza na Morocco jana wameondoka leo kwenda mkoani Kagera kwa ajili ya mechi ya Jumatano ijayo (Machi 27) dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba.Hata hivyo, walipofika Mwanza, Shirika la Ndege la Precision likatangaza kwamba Uwanja wa Ndege wa Bukoba umejaa maji kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika siku za karibuni.
Kutokana na hali hiyo, wachezaji hao watano wa Simba- Juma Kaseja, Nassor Masoud, Shomari Kapombe, Amri Kiemba na Mwinyi Kazimoto, sasa wataondoka Mwanza kesho saa sita mchana kwenda Bukoba.
Wataungana na wachezaji wengine wawili wa Simba, Mussa Mude na Abel Dhaira, ambao wanarejea Uganda leo wakitokea Monrovia, Liberia, ambako timu yao ya taifa ilicheza jana usiku.
Wachezaji wengine wa Simba wako katika hali nzuri na wanaendelea na mjini Bukoba.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

No comments:
Post a Comment