Search This Blog

Thursday, March 28, 2013

MSIMAMO WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA NA RATIBA YA MECHI ZA WIKIENDI HII - RUVU YATAMBA KUICHINJA AZAM

Maafande wa jeshi la kujenga taifa, Ruvu Shooting ya mkoani Pwani wametamba kuwamaliza Azam Fc, Lambalamba katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kupigwa uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani jumamosi ya wiki hii.

Ruvu Shooting wenye pointi 29 ,nafasi ya saba ya msimamo watashuka katika dimba lao la nyumbani kusaka ushindi ili kumaliza msimu huu wa ligi wakiwa nafasi nne za juu.

Akizungumza na mtandao huu, Afisa habari wa Ruvu shooting, Masau Bwire, amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda barabara huku kocha mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa “Master” akirekebisha makosa yaliyojitokeza mechi iliyopita ambayo walifungwa 1-0 na vinara wa ligi hiyo, klabu ya Yanga.
Masau alisema Azam fc jana walishinda 3-0 dhidi ya wapiga kwata wenzao wa Tanzania Prisons hali ambayo imewapa nguvu kubwa ya kuwania ubingwa, lakini mchezo wao wa Jumamosi wasitarajie urahisi hata kidogo.
“Wapinzani wetu wamefanya vizuri kombe la shirikisho kwa kuwafunga Barrack Young Controller II mabo 2-1 ugenini, jana wamepata matokeo mazuri mbele ya Prisons na wanazidi kuamsha mizimu ya kuusaka ubingwa, sisi tunahitaji nafasi ya kushiriki hata Tusker cup mwaka huu, hatukubali kufungwa”. Masau alitamba.
Afisa habari huyo ameongeza kuwa mchezo uliopita dhidi ya Yanga ambao walipoteza, walistahili kushinda kutokana na kiwango cha vijana wao, lakini walikosa nafasi nzuri za kufunga na wapinzani wao walipata nafasi moja waliyoitumia kupata ushindi.
Masau alisema Mkwasa anaendelea kunoa makali ya washambuliaji wake wakiwemo Hassan Dilunga, Said Dilunga, Ernest Ernest, Ayubu kitala ili kuibuka wababe katika mchezo huo wa kukata na shoka.
“Watanzania wanawajua vizuri Ruvu shooting, moto tunaowasha si mchezo, tutawapiga Azam fc na baada ya hapo tutaanza hesabu za kuwavaa Polisi Morogoro wiki ijayo”. Masu aliongeza.
Akizungumzia malengo yao kwa sasa, msemaje huyo amesema wapo nafasi ya saba na ponti 27 huku wakiwa na michezo saba kibindoni, hali hii inawapa matumaini ya kufanya vizuri na kushika hata nafasi ya nne ili kucheza kwa mara ya kwanza michuano ya kimataifa yaani kombe la Tusker linaloshirikisha klabu za afrika mashariki.
Kwa upande wa Azam fc kupitia kwa afisa habari wao Jaffar Idd Maganga wamesema kuwa mchezo  huo utakuwa mgumu sana kwao na wanauchukulia kwa umakini mkubwa sana ili kupata pointi tatu na kuendeleza harakati zao za kuwania ubingwa.
Pia alisema mchezo huo wataumia kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho dhidi ya Waliberia, Barrack Fc machi 9 mwaka huu dimba la taifa jijini Dar es salaam.
“Sisi kila mchezo kwetu ni fainali, katu hatudharau timu yoyote ya ligi kuu, tuna safari ndefu na tunakabiliwa na michuano ya kimataifa, lakini tunafanya jitihada kubwa kujiandaa kwa ajili ya mashindano yote, na jumamosi tutashinda kama jana”. Idd alisema.
Azam fc wapo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 40 huku Yanga wakiwa kileleni na pointi 48. Mabingwa watetezi simba wanabakia nafasi ya tatu na pointi 34 baada ya kupoteza 1-0  mchezo wa jana dhidi ya Kagera sugar.
Ligi kuu kwa sasa imejigawa katika makundi matatu, kundi la kwanza ni timu zinazowania ubingwa wa ligi kuu kwa maana ya Yanga, Simba na Azam fc, kundi la pili ni zle zinazowania nafasi mojawapo za juu, Mtibwa Sugar, Coastal union, kagera sugar, JKT Oljoro, Ruvu shooting na kundi la mwisho ni zile zinazowania kukwepa mkasi wa kushuka daraja, JKT Ruvu, Tanzania Prisons, Toto Africans, African Lyon.

RATIBA: Jumamosi Machi 30
JKT OLJORO v JKT RUVU [SH. AMRI ABEID, ARUSHA]
RUVU SHOOTINGS v AZAM FC [MABATINI, PWANI]
AFRICAN LYON FC v COASTAL UNION [AZAM COMPLEX, KAGERA]
POLISI MOROGORO v YOUNG AFRICANS [JAMHURI, MOROGORO]
KAGERA SUGAR v MTIBWA SUGAR FC [KAITABA, KAGERA]
TOTO AFRICANS v SIMBA SC [CCM KIRUMBA, MWANZA]

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
YANGA
20
15
3
2
25
48
2
AZAM FC
20
12
4
4
19
40
3
SIMBA
20
9
7
4
11
34
4
KAGERA
21
9
7
5
5
34
5
COASTAL
21
8
8
5
4
32
6
MTIBWA
21
8
8
5
4
32
7
RUVU SHOOTING
19
8
5
6
3
29
8
JKT OLJORO
21
6
7
8
-3
25
9
MGAMBO
21
7
3
11
-6
24
10
PRISONS
21
4
8
9
-9
20
11
JKT RUVU
18
5
4
9
-12
19
12
POLISI
21
3
8
10
-10
17
13
TOTO
21
3
8
10
-12
17
14
LYON
21
4
4
13
-18
16

1 comment:

  1. Kwa namana msimamo huu ulivyo nina maoni yafuatayo;
    1.Yanga ina wastani wa kupata pointi 2.40 kwa kila mechi moja inayocheza,Azam pointi2.00 na Simba pointi 1.70
    2.Kwa misimu mitatu mfululizo iliyopita Yanga haikuwahi kuvuka pointi 50 lakini kwa hali ilvyo msimu huu watavuka mapema pointi hizo
    3.Kuanzia timu ya 7-14 goal difference yao ni hasi au minus hali inayoonyesha tofauti kubwa ya kiuwezo kati ya timu 7 za juu na timu 7 za chini.

    3.Yanga ina wastani wa kushinda mechi 3 katika kila mechi 4 inazocheza.Azam ina wastani wa kushinda mechi 3 katika kila mechi 5 wanazocheza.Simba ina wastani wa kushinda mechi 2 katika kila mechi 4 inazocheza.

    4.Hivi sasa timu hizi tatu zimebakiza mechi sita kila moja.Yanga ikishinda mechi zote "point ceiling" yake ni pointi 66,Azam 58 na Simba 52.Kumbukan katika mechi zilizobaki Yanga ina mechi moja na Simba na pia Azam ina mechi moja na Simba na hivyo matokeo ya mechi hizi yanaweza kubabadili "point ceiling" baina ya timu hizi tatu.

    ReplyDelete