Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya soka kufunga mfululizo kwenye mechi 17 mechi za ligi, baada ya kupiga bao la ushindi kwenye mechi ya jana kati ya Barcelona na Deprotivo La Coruna.
Goli la jana la Messi ambalo liliipa Barca ushindi wa 2-0 dhidi ya Galicians, limemfanya Messi avunje rekodi ya Teodor Peterek aliyefunga mabao 16 mfululizo.
Peterek alifunga mabao 22 kwenye 16 mechi za ligi kuu ya Poland kwenye msimu wa 1937-38.
Messi, ambaye hivi karibuni alivuka rekodi ya kufunga mabao 200 ya La Liga, sasa hivi amefikisha mabao 40 kwenye La Liga msimu huu, mabao ambayo yangemfanya aweze kushinda tuzo ya Pichichi kwenye misimu yote ya La liga kasoro msimu uliopita - ambayo alishinda mwenyewe.
Mshambuliaji wa zamani wa Brazil Ronaldo huko nyuma aliweka ya kufunga kwenye mechi 10 mfululizo wakati akiwa na Barca, rekodi ambayo imevunjwa na Messi.
No comments:
Post a Comment