Search This Blog

Tuesday, February 26, 2013

YANGA NA AZAM WAZIFUNIKA SIMBA NA MTIBWA KIMAPATO

Katika mechi zilizochezwa wikiendi iliyopita zilizowahusisha watani wa jadi Simba na Yanga, zilizocheza mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na Azam mapato yaliyopatikana kutokana na viingilio hizi yametolewa hadharani kama kawaida. Na kama ilivyokuwa huko nyuma Yanga imeendelea kuipeleka Simba kwa kuingiza fedha nyingi kutokana kwenye mechi zinazoihusisha klabu hiyo ya jangwani.

Wakati katika mechi kati ya Simba na Mtibwa ikiingia millioni 62, mechi ya Yanga na Azam imeingiza 240.
  
  MECHI YA SIMBA, MTIBWA YAINGIZA MIL 62/-
Mechi namba 121 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 24 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Mtibwa Sugar kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba imeingiza sh. 239,686,000.

Watazamaji 10,669 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,577,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,467,694.92.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 9,491 na kuingiza sh. 47,455,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 105 na kuingiza sh. 2,100,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,412,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,447,297.36, Kamati ya Ligi sh. 4,447,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,223,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,729,504.53.

MECHI YA YANGA, AZAM YAINGIZA MIL 240/-
Mechi namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.

Watazamaji 39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 6,975,669.36.


3 comments:

  1. Wanasoka naomba tujadili gharama za mechi, nataka nijue uhusiano wa ongezeko la watazamaji na gharama za mechi, ninachojua gharama za mechi zinapangwa kabla ya mechi kuanza, sasa sijajua ongezeko la mtamaji linahusiana vipi na ongezeko la gharama, naomba kueleweshwa kidogo inawezekana sijui hizi gharama ni kitu gani

    ReplyDelete
  2. angalieni idadi ya watazamaji na na mapato huwezi kupata pesa nyingi kama huna watu

    ReplyDelete
  3. naomba Shaffih unisaidie katika mgawanyo wa mapato kwa kulinganisha na nchi za wenzetu hususani ulaya..kwa mawazo yangu naona klabu zetu ambazo ndo wavuja jasho wanapata kiduchu..ebu nisaidie kitakwimu kama mtazamo wangu ni sahihi.

    ReplyDelete